Monday 9 January 2017

Kwanini Huna Furaha

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na unaendelea vizuri kusonga mbele kuyatafuta mafanikio.

Karibu sana katika makala ya Leo inayosema ""kwanini huna furaha". Leo ni jumatatu ni siku mpya ni siku ya kwanza katika wiki.Lakini ni siku ambayo watu wengi wanaichukia kupita siku nyingine sita zinazobaki. Wengine wanaiita "blue Monday".

Sitaki niende mbali na mada yangu usije ukapotea. Sababu kubwa ya watu wengi kutokuwa na furaha ni uoga. Utakuta mtu hana furaha dhidi ya mtu anayempenda hii ni kwa sababu ana uoga wa kuachwa. Mwingine hana furaha na kazi yake sababu hanaogopa kuachishwa kazi.

Bofya hapa kusoma; Ulipo ni mahali sahihi

"Jambo la kuogopa ni kuogopa" alisema F.J .Kennedy raisi wa zamani wa Marekani.

Uchunguzi uliofanya unasemekana kwamba watu wengi huwa hawana furaha inapofika jumapili kuelekea jumatatu. Hii ni kwa sababu ya woga. Mwingine anawaza wiki hii atakuwa na kazi nyingi ofisini. Mwingine anawaza anarudi kwenye kazi inayomchosha. Mwanafunzi anaanza kuwaza yule mwalimu mkali au hajafanya kazi yeyote. Ukichunguza kwa undani hayo yote ni mambo yaliyojaa uoga ndani yake.

Bofya hapa kusoma; sababu 7 zitakazo kufanya uwe na furaha muda wote.

Jaribu kuchunguza wewe mwenyewe chanzo cha wewe kukosa furaha ni nini. Bila kupoteza muda utakuta ni uoga unaopanda kichwani mwako.

Kumbe hatuna budi kuzika uoga ili tuweze kuwa na furaha ndani mwetu. Zika uoga zidi ya kazi yako. Zika uoga zidi ya masomo yako. Zika uoga katika kila kitu ambacho wewe unakifanya. Na utajikuta muda mwingi unakuwa mtu wa furaha.

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu.
Edius Bide Katamugora

Tuwasiliane;
0764145476.
Whatsapp; 0625951842 (Tuma neno "SUBSCRIBER" niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja).
Email: ekatamugora@gmail.com
Facebookpage: bideismblog
Instagram: @eddybide

Asante kwa kuwa na Mimi bega kwa bega. Usisite kuwashirikisha na wenzako kile unachopata hapa.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: