Saturday 11 March 2017

Kanuni Ya 20-40-60

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama. Leo ni siku muhimu sana ambayo tukiitumia vizuri.

Karibu sana kwenye mgodi huu wa ufahamu. Nipende moja kwa moja kwenda kwenye Makala yetu ya leo ambapo tutajifunza kanuni muhimu sana katika maisha yetu. Kanuni inayoitwa "Kanuni ya 20-40-60 (The 20-40-60 rule).

Mara nyingi kitu kinachowarudisha watu wengi nyuma ni maneno " watu watasema au watanifikiriaje " hili ni jambo ambalo muda mwingi linatufanya tusifanye mambo tuliyoyapanga kwa hofu ya watu watasema nini.

Unakuta mtu anakipaji,lakini hawezi kukionesha kwa hofu ya watu watasema nini.

Mwingine labda anataka kurudi shule ukubwani lakini kwa sababu ya hofu ya watu watasema nini juu yske anaamua kuagaili jambo hilo la kusoma.

Au mwingine labda ni mnene,anaogopa kuanza mazoezi kisa watu watasemaje,bosi wake atasemaje,wafanyakazi wenzake watasemaje. Hivyo anaamua kuacha.

Leo nataka nikupe dawa ambayo ni dozi halisi ya fikra yenye sumu Kali iliyo na makazi vichwani mwa wengi.

Dawa hiyo ni kanuni ya 20-40-60,iliyowekwa na muigizaji wa kike anayeitwa Shirley Maclane. Kanuni hiyo inasema hivi;

"Ukiwa na miaka 20, muda mwingi huwa unahofia watu wengine wanakufikiriaje".

"Ukiwa na miaka 40, unashtuka na kusema,sijali watu wengine wanasema nini kuhusu Mimi".

"Ukifikia miaka 60,unagundua hakuna anayefikiria kuhusu wewe hata kidogo" .

Kanuni hii inatufundisha kwamba "kutoka mwanzo hakuna mtu yeyote anayetufikiria", kila mtu anafikiria mambo yake.

Boss wako hakufikirii we we.
Marafiki zako hawakufikirii wewe.    Ndugu zako hawakufikirii wewe.

Ijue sasa kanuni hii na itakusaidia kutimiza malengo yako. Kutilia mkazo Dan Kennedy aliwahi kusema "Your opinion of you is far more important than anyone else’s or everyone else's" akimaanisha "maoni yako juu yako ni muhimu zaidi kuliko ya mtu mwingine yeyote.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
0764145476
0625951842
Email: ekatamugora@gmail.com

Asante kwa kusoma Makala hii na karibu tena. Usisite kuwakaribisha na wenzio.

"See you at the top" .

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: