Tuesday 9 May 2017

Habari mpendwa msomaji wa makala hizi za Bideism blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya. Nikukumbushe yakwamba Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia. Leo nataka niongelee kulizika. Mpendwa rafiki yangu, unapoanza kusema inatosha ndipo unapoanza kurudi nyuma kule ulikotoka. Kama ukikuwa msomaji mzuri wa Makala ukisema Makala nilizosoma zinatosha utajisahau na kurudi Kule ulikotoka.

Ukiwa msomaji wa Vitabu na kusema inatosha kwa Vitabu nilivyosoma utakuwa unapoteza maarifa mengi ambayo ungeyapata siku zinazokuja hivyo utapotea.

Jifunze kutokulizika. Ukifanikiwa kumaliza jambo moja unaanza jingine, ndiyo maana hata kwenye mashamba ukitoa mahindi unaweka viazi, ukivuna viazi na unapanda mihogo. Kama ukiacha kupanda na kusubiri msimu wa mahindi tena utaishi katika ukata.

Bwana Thomas Edson aliwahi kusema "show me a satisfied man, I will show you a failure" akimaanisha "nioneshe mtu aliyelizika, nikuoneshe mtu alyeshindwa." Kumbe tunapolizika tunaanza kurudi kwenye kushindwa. Acha kulizika. Safari moja uanzisha nyingine.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Author and Motivational Speaker
0764145476
0625951842
Email:ekatamugora@gmail.com

Usisite kulike page yetu ya Facebook hapa chini na kujiunga na mfumo wetu wa email.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: