Monday 29 May 2017

Huduma Nzuri Ni Biashara




Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kwenda kutimiza majukumu yako ya leo na kuongeza kitu Fulani kitakacho kusaidia kutimiza ndoto zako. Leo ni siku muhimu sana usikubali ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana katika Makala nzuri ya leo niliyokuandalia.
Leo hii ningependa kuongelea kitu muhimu katika biashara na ujasiriamali. Kitu hicho ni HUDUMA. Wafanyabiashara wengi na wajasiriamali wengi hasa wale wanaoanza biashara, biashara zao huanguka na kurudi nyuma kwa sababu hawalizingatii jambo hili. Wengi wanatanguliza pesa kwanza na kusahau kutoa huduma bora.

Leo nataka nikwambie kwamba hakuna kitu muhimu kwenye biashara kama huduma unayoitoa kwa wateja wako. Ukiwa kama mjasiriamali au mfanya biashara tanguliza kwanza huduma na pesa zifuate. Toa huduma bora, uziwe mtu wa kuwaza pesa kabla ya kuwapa wateja wako huduma nzuri.
Watu wengi wamekuwa wakiyaamini makampuni makubwa na kuwa wateja wa kampuni hizo kwa sababu ya huduma nzuri wanazozipata kutoka kwenye kampuni hizo. Ingawa wakati mwingine kampuni hizo zinawatoza pesa nyingi lakini wajikuta wanalipia kiasi kizuri kwa sababu ya huduma nzuri wanazozipata.

Umewahi kufikiria kwanini kuna hoteli baadhi wanauza glasi ya juisi ya embe kwa shilingi elfu tano na sehemu nyingine glasi kama  hiyo hiyo ya embe wanauza shilingi mia tano na watu wapo tayari kwenda kununua sehemu wanakouza elfu tano na kuacha sehemu inapouzwa juisi kama hiyo kwa shilingi mia tano.

Faida ya kutoa huduma nzuri ni kwamba watu watakuja kwako tu ingawa muda mwingine unakuwa na bei za juu kuliko wenzako. Kuna mtu aliwahi kusema “Give good service to all people and when they come, bill them.” Akimaanisha, “Toa huduma nzuri kwa watu na wakija kwako kununua watoze pesa.”

Faida nyingine ya kutoa huduma nzuri ni kwamba utaongeza wateja. Hii ipo hivi, akija leo mtu Fulani kwenye biashara yako ukampa huduma nzuri, atakwenda kuwaambia wenzake huduma nzuri unayoitoa, na wateja wataanza kuja kwako kuangalia kama kweli unatoa huduma nzuri waliyoambiwa. Wakija na kukuta jambo waliloambiwa linatendeka, watakuwa wateja wako pia, hivyo hivyo watawaambia na wengine.
Wafanya biashara wengine wamekuwa na tabia za kutapeli, wamesahau kwamba dunia ni duara. Utamtapeli mtu hapa leo na utakwenda kukutana nae sehemu nyingine. Usiwahi kufanya biashara ya dhuruma hata siku moja, hapo pia unajiwekea mikosi katika biashara zako.

Wajasiriamali na wafanya biashara wengine wamekuwa wakijisahau kidogo, yaani wanaanza na huduma nzuri na baada ya kupata pesa wanasahau kile wanachokifanya na kuacha kutoa huduma nzuri. Kumbuka watu walikuja kwenye biashara yako kufuata huduma nzuri na si vinginevyo. Kama ni mama nitilie, watu walikuja kwako kwa sababu tu ulikuwa ukipika chakula kitamu na kizuri. Wataondoka kwako endapo utabadili ladha na kuanza kupika ovyovyo. Kama ni fundi viatu, watu walikuja kwako kwa sababu tu ulikuwa ukiwashonea viatu vyao vizuri, lakini leo umekuwa ukifanya ilimradi tu liende, wateja wako watakukimbia. Hii inatumika kila mahali kwenye biashara yeyote.

Kwenye kitabu kinachoitwa “Marketing Insights From A To Z”, mwandishi Philip Kotler, ameanza na maneno haya kwenye utangulizi, “Tatizo kubwa leo hii katika bishara, sio kukosekana kwa bidhaa bali ni kukosekana kwa wateja.” Na wateja wanakosa kwasababu ya huduma mbovu zinazotolewa na wafanya biashara na wajasiriamali katika shughuli zao.

Daima kumbuka kutoa huduma nzuri kwanza halafu baadaye ndipo pesa ifuate, usibadili fomula hii kwenye biashara yako, toka unapoanza na kila siku kumbuka jambo hili.

Ni mimi rafiki na ndugu yako
EDIUS BIDE KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842 (Whatsapp)

KARIBU SANA KUWEKA ODA YA KITABU CHANGU KIZURI KINACHOITWA “BARABARA YA MAFANIKO”. NI KITABU KIZURI KINACHOONGELEA MENGI KUHUSU MAFANIKIO.

Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza, kwani ni muhimu kwao pia.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: