Friday 12 May 2017


Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na huko tayari kwenda kutimiza majukumu yako siku ya Leo.

Karibu sana katika makala nzuri niliyokuandalia Leo hii.

Kuna wakati unafika na kuona ndoto zako kama zinafifia au kufa. Usikate tamaa endelea kukazana, songambele.

Dhamilia kushinda, lenga kushinda siku zote. Watu wakikwambia jambo Fulani haliwezekani. Pambana kuhakikisha wanalokwambia ni uongo. "Njia ya uhakika ya kutoshindwa ni kudhamilia kushinda." alituasa Richard Brinsley Sheridan

Unaweza kuwa na ndoto kubwa. Unaweza kuwa na malengo makubwa lakini watu wakakukatisha tamaa. Dunia ya Leo tunayoishi imezungukwa na watu wanaokatisha tamaa kuliko wale wanaopenda tufanikiwe.

Katika Biblia tunasoma hadithi ya Yozefu ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa kiongozi. Baada ya kuwahadithia ndoto hiyo ndugu zake. Walimchukia na hatimaye wakamuuza utumwani misri. "Usiku mmoja Yozefu aliota ndoto, lakini alipowasimulia ndugu zake, wao wakazidi kumchukia." (Mwanzo 37:5). Ukiwa na ndoto kubwa utachukiwa lakini usikate tamaa. Yozefu alifanikiwa.

Unapokuwa katika wakati mgumu usikate tamaa pia. Hata barabara ndefu vipi haikosi kona, haikosi mabonde, milima na kadhalika. Kamanda mmoja wa majeshi alijificha pangoni baada ya jeshi lake kushindwa. Alipokuwa pangoni alimuona mdudu akiwa amebeba chakula anajaribu kupanda jiwe. Mdudu huyo alidondoka Mara Tisa akiwa amebeba chakula. Mara ya kumi mdudu huyo alifanikiwa kupanda jiwe. Askari huyo alivyoona mdudu huyo alivyofanikiwa alitoka nje ya pango na kurudi uwanja wa mapambano.

Unaposhindwa jifunze kutokana na makosa. Endelea Mbele utafanikiwa.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Author & Motivational Speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com

Usisahau kujiunga na mfumo wetu wa email hapa chini na pia kulike page yetu ya Facebook.

Washirikishe na wenzako pia.

See You At The Top

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: