Friday 23 June 2017

Faida Utakazozipata Baada Ya Kusoma Kitabu Cha Barabara Ya Mafanikio

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri kujishughulisha na kupambana kuelekea mafanikio. Nikukumbushe tu leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako usikubalii ipotee hivi hivi. One day can make you grow. 
 
Baada ya kuandika kitabu ambacho kimegusa maisha ya watu wengi hasa Wale walioobahatika kukisoma kitabu cha Barabara Ya Mafanikio. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiniuliza swali kwamba kitabu kinahusu nini. 

Baada ya kupata swali hilo mara nyingi tu nimeamua kuandika makala haya kwa ajili ya watu wengine ambao wangependa kujua nimeandika kuhusu nini.

Kwanza kabisa jambo ambalo unapaswa kulitambua ni kwamba kitabu cha barabara ya mafanikio kimegusa maisha ya kila mtu. Kuanzia mtoto, kijana, mzazi, mwanafunzi, mjasiriamali, mwajiriwa, mwajiri, mfanyabiashara, kutaja wachache.

Zifuatazo ni faida utakazozipata baada ya kusoma kitabu cha barabara ya mafanikio:

Mtizamo:
Mwandishi anaamini kwamba watu wakibadili mtizamo wao na kuwa na mtizamo chanya, watapata mafanikio ya haraka. Hivyo amejitahidi sana kukuandikia namna ya kubadili mtizamo wako kutoka hasi hadi chanya.

Fursa :
Mwandishi amejitahidi kueleza fursa mbalimbali ambazo mtu anaweza kuzitumia kujipatia kipato na pia baadhi ya maandiko yamekwisha anza kutumiwa kama fursa. Baada ya kumpatia rafiki yangu Hamisi ambaye anapenda sana muziki wa rap na anaimba pia nakala ya kitabu cha barabara ya mafanikio aliweza kupata kanuni moja muhimu ambayo nimeiandika humo na hatimaye akasema albamu yake ataiita jina la kanuni hiyo. Kumbe kitabu hichi ni fursa pia. Ukipata muda wa kukisoma utajua kanuni hiyo.

Malezi ya watoto.
Mafanikio ya mtu yanaanza akiwa bado mtoto mdogo ingawa wengine wanachelewa kwa sababu ya mazingira waliokulia, hivyo basi kitabu hiki kinaeleza ni kwa jinsi gani wazazi wanaweza kuwalea watoto wao kwenye maisha bora na yenye mafanikio tele. "Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee." (Mithali 22; 6)
Vipaji na kusudi:
Kila mtu ameletwa duniani ili kutimiza kusudi fulani na pia kutumia vipaji na vipawa alivyojaliwa ili kufikia mafanikio ya juu kabisa. Mwandishi ameeleza ni kwa namna gani mtu anaweza kutambua vipaji na pia kusudi lake. Ikumbukwe pia mwandishi ni fundi katika maswala yanayohusu vipaji kwani ndiye mwanzilishi wa group la whatsapp lenye watu zaidi ya 100 linaloitwa Whatsapp Talent School (WTS)

Biashara na Ujasiriamali:
Biashara na ujasiriamali ni vitu ambavyo vinaweza kukuletea mafanikio ya kiuchumi haraka Sana zaidi ya kitu kingine chochote kinachohusu fedha. Hivyo mwandishi ameelezea biashara zinawezaje kupata wateja wengi na wenye faida. Mbinu mbalimbali za kuwahudumia wateja na namna ya kuziona fursa mbalimbali kama mjasiriamali.

Mitandao ya kijamii:
Mitandao ya kijamii ni kitu ambacho hakiepukiki katika karne ya ishirini na moja. Kitabu cha barabara ya mafanikio kinaeleza jinsi mtu anavyoweza kujiingizia kipato kwa kutumia mitandao hiyo. Unaweza kuonesha kipaji biashara na vitu vingi ulivyonavyo kwa kutumia simu yako ya mkononi kumfikia kila mtu katika sekunde moja dunia nzima. Haya yote utayapata ndani ya kitabu cha barabara ya mafanikio.

Elimu:
Mwandishi wa kitabu hiki ni mwanafunzi, ingekuwa dhambi kubwa kuandika kitabu na kuacha kugusia sekta nyeti kama ya elimu. Hivyo kwa mwanafunzi yeyote wa shule yeyote au chuo hana budi kupata nakala ya kitabu cha barabara ya mafanikio kwani kitamsaidia sana katika masomo yake. Na hata baada ya masomo katika swala zima la kutafuta ajira.

Maendeleo binafsi :
Mafaniko yanahusu pia maendeleo binafsi katika maisha ya kila mwanadamu. Hivyo mwandishi amegusa kabsa maisha ya kila siku ya jamii zinazotuzunguka na jamii anayoishi kila mtanzania wa Leo.

Usifanye kosa mwaka huu kuisha bila kusoma kitabu hiki cha barabara ya mafanikio.

Baada ya Wiki 2 kutoka kitabu hiki bei yake itapanda kutoka 6000/= hadi 10000/= hivyo ni bora kuweka oda na kupata kitabu chako mapema iwezekanavyo kwa bei ya chini kabisa.

Nikikukumbushe kwamba kitabu hiki ni muhimu na kinagusa maisha ya kila mtu.

Mafanikio yapo mikononi mwako

Ndimi
Edius Katamugora (Bide)
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya facebook hapa chini (bideism blog).

Karibu pia kuweka oda ya kitabu changu kizuri cha Barabara Ya Mafanikio kwa mawasiliano yangu hapo juu.

Washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: