Wednesday 7 June 2017

Huitaji Umri Mkubwa Kufanya Makubwa

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog.  Tumshukuru Mungu kwa siku nzuri kama ya Leo. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza ndoto zako siku ya leo. Leo ni siku muhimu husikubali ipotee.

Karibu sana katika makala nzuri ya Leo niliyokuandalia.
Watu wengi wamekuwa na mawazo na fikra ya kwamba ili mtu afanikiwe lazima awe na umri fulani mkubwa,  tuseme labda miaka thelathini na kuendelea.  Ukweli ni kwamba, huhitaji umri mkubwa kufanya mambo mkubwa.

Kitu unachohitaji ni kuwa na nguvu na uwezo wa kuthubutu hata ukiwa na umri mdogo tu. Kitu kikubwa ni kuweka hofu pembeni na kusonga mbele. Kila kitu kinawezekana.  Napoleon Hill aliwahi kusema "niliponunua kamusi yangu neno la kwanza kufuta ni 'haiwezekani'(impossible) "

Ukifuatilia kwa ukaribu watu waliofanikiwa na kuwa matajiri wakubwa wengi walianza wakiwa na umri mdogo wengi wakiwa na umri wa miaka kumi na kitu.

Kwenye kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio nimeandika kuhusu Tajiri namba moja duniani Bwana Bill Gates.  Bill Gates aligundua mchezo wa kompyuta (game) akiwa na umri wa miaka 11, baadaye akaja kufungua kampuni ya Microsoft pamoja na mwenzake Paul Allen(19) yeye akiwa na miaka 16.

Nimewahi pia kusoma kuhusu mtoto mmoja wa Kimarekani anayeitwa Mikaila. Mtoto huyu wa like ana umri wa miaka 12 lakini anamiliki kampuni yake.  Ameweza kuanzisha kampuni inayotengeneza juisi ya limao iliyochanganywa na asali. Juisi hiyo iliyowekewa lebo ya "me and the bees-lemonade" Imeifanya brand yake ikue kwa haraka sana na kuuza kwenye zaidi ya nchi ishirini duniani. Amekuwa akifuga nyuki na kuvuna asali mwenyewe pamoja na umri wake mdogo. Wazazi wake wamemsaidia sana kutimiza ndoto zake katika biashara, hasa baba yake anayefanya kazi kwenye kampuni ya Dell. Siku moja Raisi mstaafu wa Marekani akiwa anatoa hotuba alimkaribisha mtoto huyo kutoa neno kidogo kwa wananchi.  Mtoto huyu alipanda jukwaani na kumkumbatia raisi Obama na baadaye kusema maneno haya "Kujifunza biashara ni kitu rahisi, anza kwa kuondoa hofu iliyoko ndani mwako."

Jiulize Leo wewe kijana mwenzangu kama wenzako wameweza,  kina Mikaila, Bill Gates na wengine, kwanini mimi nisiweze?

See you at the top

Ni mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Author and motivational Speaker
0625951842 (Whatsapp)
0764145476
ekatamugora@gmail.com

KARIBU SANA KUWEKA ODA YA KITABU CHANGU KIZURI CHA "BARABARA YA MAFANIKIO" BEI NI SHILINGI 10000.

Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza.

Tukutane kesho katika mwendelezo wa makala hii. Asante kwa kuwa mdau mkubwa wa Blogu hii.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: