Monday 26 June 2017

Jiconnect Watu Wakuconnect

Mara nyingi watu wengi wamekuwa wakilalamika kwamba wanakosa connection ambazo zingeliwawezesha waweze kupata kitu walichokinuia, kama ajira n.k

Kitu muhimu ambacho ningependa ujifunze Leo ni kwamba connection unazitengeneza wewe mwenyewe.

Wengine wamebaki kulalamika au kuwalalamikia baadhi ya watu kwa kuwanyima connection ambazo zingewawezesha kufanikiwa haraka.
Utasikia mtu akisema, mimi sina connection hivyo siwezi kufanya kitu Fulani, siwezi kupata kazi fulani.

Jambo ambalo nataka ujifunze leo ni kwamba wewe ni connection tosha kama ukihamua kujijenga, wewe ni connection tosha kama ukihamua kubadilika.
Mhasishaji Jim Rohn aliwahi kusema "kama ukibadilika, kila kitu kwenye maisha yako kitabadiliki. "

Mpendwa msomaji, kama unakipaji au uwezo Fulani mkubwa ambao tayari umeanza kuuonesha, huwezi kukosa connection unayoitaka. Watu wanatoa connection kwa kuangalia wewe una nini ndani mwako kitakachomsaidia huyo anayekupa connection.

Hakuna mtu atakayekubali kukupa connection kama wewe huna kitu kitakachomsaidia.
Hivyo leo usibaki kulalamika eti huna connection kama huna kitu kitakachomshawishi mtu ajiunganishe na wewe.

Kanuni ya asili ya uvutano inasema "vitu vyenye asili inayofatana uvutana. " Kumbe mtu atakupa connection unayoitaka kwa kuona kwamba una kitu ambacho kitamsaidia yeye pia aendelee na sio ashuke kimaendeleo.

"Connection unaanza kuzitengeneza wewe kwa kuweka mazingira bora ili watu
wakupe connection. "- Edius Katamugora

Mafanikio yapo mikononi mwako.

Ndimi
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya facebook hapa chini (bideism blog). 

Karibu pia kuweka oda ya kitabu changu kizuri cha Barabara Ya Mafanikio kwa mawasiliano yangu hapo juu.

Washirikishe na wenzio kile ulichojifunza

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: