Kuna tofauti kubwa kati ya kutaka kitu na kuwa tayari kukipata.
Asilimia kubwa ya watu wanataka mafanikio lakini hawapo tayari.
Unataka kufaulu vizuri katika mitihani yako. Je hupo tayari kusoma kwa bidii, kuamka usiku wa manane usome vitabu ambavyo hata mwalimu wako hajawahi kutumia huku ukitafuta maarifa zaidi. Watu wengi wanataka lakini hawako tayari.
Unataka kuwa mwandishi wa vitabu na makala nzuri. Je hupo tayari kuamka alfajiri na mapema kuandika chochote cha kuelimisha jamii. Je hupo tayari kujitoa kuandika makala yoyote karibia kila siku.
Unataka kufanya kilimo cha umwagiliaji maana umesikia kinalipa?. Je upo tayari kufanya umwagiliaji mara tatu kwa siku?.
Unataka uanze biashara? Je upo tayari kuielezea biashara yako mbele ya watu na wakaweza kununua kutoka kwako au ndo umejawa na aibu. Unawaogopa watu.
Mpendwa msomaji, kama na wewe hupo kwenye kundi la wanaotaka,badilika na uwe na utayari. Watu wengi wanakosa moyo wa utayari ndiyo maana hawafanikiwi.
Zakayo mtu mfupi na tajiri sana aliposikia Yesu akipita mahali alipokuwa akiishi, alitaka kumuona lakini alishindwa kwa sababu alikua amezungukwa na kundi kubwa la watu. Hiyo haikuwa shida kwake Zakayo aliamua kupanda mti. Yesu alipofika mahali pale alimwambia "Zakayo shuka mti Leo nataka kushinda nyumbani kwako." Huyu ni mtu aliyeonesha utayari wake pamoja na kuwa mfupi akitaka kumwona Yesu, njia pekee ilikuwa ni kupanda mti.
Tunajifunza nini hapa?
Jambo la msingi tunaloweza kujifunza hapa ni kwamba ukitaka kufanikiwa katika jambo Fulani lazima uwe na utayari ndani mwako. Watu wenye utayari ni watu wanaosema liwalo na liwe nakomaa mpaka kieleweke.
Jambo la msingi tunaloweza kujifunza hapa ni kwamba ukitaka kufanikiwa katika jambo Fulani lazima uwe na utayari ndani mwako. Watu wenye utayari ni watu wanaosema liwalo na liwe nakomaa mpaka kieleweke.
Watu wenye utayari ni watu wasiokata tamaa. Ni watu wanaoona mteremko mahali palipo na mwinuko na milima.
Usiishie tu kutaka bali kuwa tayari. Watu wengi wanataka, lakini hawapo tayari. Jitofautishe Leo. Ukisema nataka kufanikiwa sema nipo tayari kufanikiwa.
Henry Ford mmiliki wa kampuni inayotengeneza magari ya Ford. Aliwaambia mainjinia/wahandisi wake watengeneze gari lenye silinda 8. Mainjini a wakamwambia haiwezekani. Akawaambia endeleeni na utafiti lakini walirudi na kumwambia haiwezekani. Akawarudisha tena na kuwaambia inawezekana. Baadae walifanikiwa kutengeneza injini yenye silinda 8. Isingelikuwa utayari wa Henry Ford nafikiri magari aina ya V8 yangelikuwa bado hayajavumbuliwa. Ni utayari wa Henry Ford kusema inawezekana uliopelekea jambo hilo kutendeka. Unahitaji kuwa na utayari pia katika mambo unayotaka kuyafanya.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapatikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842
Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment