Thursday, 8 March 2018

Watu Watanionaje Inakuchelewesha

Kuna watu wengu wanandoto kubwa na malengo makubwa lakini kitu kinachowarudisha nyuma in kuanza kufikiri watu watawaonaje au kuwasemaje.

Maisha yao yamekuwa yakiongozwa na watu wengine wala si wenyewe. Watu was namna hii ni watu ambao bado hawajatambua nguvu kubwa na za ajabu walizozibeba.

Nimeona na nimekutana na watu wengi wanaogopa kufanya mambo wanayotakiwa kufanya kwa kuogopa watu watawasemaje na watu watawaonaje.

  • Kuna watu wanaogopa kuanza  kusoma masomo ya jioni wakiogopa wafanyakazi wenzao watawaonaje.
  • Kuna watu wanaogopa kurudi shule kuendeleza kisomo  chao wakiogopa jamii inayowazunguka itawaonaje.
  • Kuna watu hawataki kabisa kutumia vipaji vyao walivyopewa wakiogopa na kusema watu watawaonaje na kuwasemaje.
Mpendwa msomaji usipokuwa mtu wa kufanya maamuzi huwezi hata siku moja kupiga hatua yoyote.

 
(Kupata kitabu pichani, piga 0764145476.)

Watu hata wakikusema vibaya vipi hilo haliwezi hata kukupunguzia kilo kwenye mwili wako, utabaki yuleyule. Jambo la msingi ni kupiga moyo konde na kuendelea mbele.

"Watu milioni 50 wakisema jambo la kipumbavu bado la kipumbavu," alisema Anatole France (1844-1924). Kumbe wingi wa watu watakaokusema vibaya haujalishi. Kama wanasema uongo hata siku moja wingi wao hauwezi kubadili uongo kuwa ukweli.

Kwenye kitabu changu cha BARABARA YA MAFANIKIO niliongelea kanuni ya 20-40-60 iliyowekwa na muigizaji wa kike Shirley Maclaine inayosema:

"Ukiwa na miaka 20, muda mwingi huwa unahofia watu wengine wanakufikiriaje.

Ukiwa na miaka 40, unashtuka na kusema, sijali watu wengine wanasema nini kuhusu mimi.

Ukifikia miaka 60, unagundua hakuna mtu yeyote anayekufikiria, kila mtu anafikiria mambo yake."

Bosi wako hakufikirii wewe. Marafiki zako hawakufikirii wewe. Ndugu zako hawakufikirii wewe. Wafanyakazi wenzako hawakufikirii wewe. Jamii inayokuzunguka haikufikirii wewe.

Leo hii amka katika usingizi mzito wa kufikiri watu watanionaje na kukusema maana unajirudisha nyuma huwezi kamwe kusonga mbele.

Jambo la kukumbuka pia ni kwamba hata ufanye jambo zuri vipi watu lazima watakusema tu. Kuna mtu aliwahi kusema "Ili kukwepa kusemwa, usifanye lolote, usiwe yeyote."

Nilipoanzisha BIDEISM BLOG sikujali watu watanisemaje ingawa kuna walionikatisha tamaa lakini sikuwa kurudi nyuma.

Nilipoamua kuandika kitabu cha BARABARA YA MAFANIKIO kilichogusa maisha ya watu wengi, kuna mtu aliwahi kuniambia "Wewe ni kichaa. Watu hawatakisoma." Lakini hilo kwangu lilikuwa kama teke analopigwa chura, maana siku zote umsogeza mbele zaidi.

"Ili kukwepa watu wasikuseme, usifanye lolote, usiwe yeyote."

Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji.
0764145476
0625951842 (WhatsApp).
Email: ekatamugora@gmail.com

Imani yangu ni kuwa Mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Washirikishe na marafiki zako ujumbe huu.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: