Friday 23 March 2018

MVUMILIVU HULA MBIVU




Kukosa uvumilivu ni kitu kilichowafanya watu wengi kuukosa utaalamu. Watu wengi hukata tamaa ndani ya muda mfupi kutokana na kupata matokeo ambayo hawakuyatarajia. Ili uwe mtaalamu unahitaji kuwa na uvumilivu wa hali ya juu. Wataalamu si watu wanaofanana na yule sungura aliyeshindwa kufikia mkungu wa ndizi na kuanza kusema, SIZITAKI MBICHI HIZI. Hasha ni watu wasiokata tamaa, ni watu wanaojua kwamba nyakati ngumu hazidumu bali watu wagumu ndio wanaodumu.

      



Maisha yetu ya kila siku yanahitaji uvumilivu bila uvumilivu maisha hayaendi. Mbuyu tunaouona ukiwa mkubwa upo leo kwasababu ya mbegu iliyoweza kuingia ardhini na kuvumilia shida zote kama kukosa maji na mengineyo, mtoto anazaliwa kwasababu mama yake aliweza kuvumilia na kuitunza mimba ndani ya miezi tisa. Bahari shwari haitoi wanamaji hodari. Watu mashuhuri, hodari na hodari ni watu walioweza kuvumilia na hatimaye leo tunawaona na muda mwingine kuwachukulia kama watu wa mfano.

Bwana mmoja alikuwa akimiliki mgodi wa dhahabu, baada ya kuchimba kwa muda Fulani alishutuka baada ya kuona haoni madini ya dhhabu tena. Hivyo aliamua kumuuzia kijana mmoja machachari. Kijana huyo hakuwa kama vijana wengine. Aliamua kwenda na kuwatafuta wataalamu wa madini waje kuchunguza eneo lile. Wataalamu wale walitoka na majibu kuwa ardhi hile bado ilikuwa na dhahabu ya kutosha. Baada ya kuanza kuchimba futi tatu kutoka bwana wa kwanza alipoachia, walikutana na bahari ya dhahabu.

 Anafanikiwa yule anayevumilia anashinda yule anayevumilia. Anakuwa mtaalamu yule anayevumilia.  “Mashindano ya mbio hashindi mwenye mbio.” (Mhubiri 9:11)

TANGAZO
Weka Oda yako ya Kitabu cha NAMNA YA KUWA MTAALAMU UKIWA BADO UNASOMA. Watu 100 wa kwanza kuweka oda watajipatia kitabu hicho kwa shilingi 5000/= tu baada ya hapo kitapatikana kwa shilingi 10000/= Kitabu hicho kitapatikana kwa njia ya NAKALA TETE utatumiwa kwa njia ya barua pepe (email) yako. Wahi sasa nafasi ni chache.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi
EDIUS KATAMUGORA
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
ekatamugora@gmail.com 

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: