Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umepata fursa ya kuiona siku nyingine yenye mchango mkubwa katika maisha yako na mafanikio kiujumla.
Karibu katika makala ya Leo inayozungumzia " Namna bora ya kubadili maisha yako''. Ili ubadili maisha yako soma vitabu.
Jitahidi kuwa msomaji mzuri wa vitabu kwani vinasidia kuongeza upeo na kuzidi kutupa elimu zaidi kuhusu maisha yetu. Vitabu ni chanzo kikubwa cha hekima. Na ukiwauliza watu wengi njia ya kufanikiwa watakwambia soma vitabu.
Kwanini kusoma vitabu?
Ninaposema kusoma vitabu simaanishi vitabu vya darasani la asha na maani vitabu vitakatifu kama vile Biblia na Kurani na vitabu vya kutia amasa (inspirational books).
Mwandishi Ben Carson anasema " ukisoma vitabu unajiunganisha na watu wakubwa wa wazamani''. Utasoma kuhusu wakina Edson Thomas, Steve Jobs, Gandhi, Nyelele, Mandela, Mother Theresa na wengine wengi.

Pia kwenye vitabu utakutana na watu maarufu kila siku ambao hukuwahi kuzani hata kukutana nao, ni kwenye vitabu tunakutana na kina Donald Trump, Ben Carson,Bill Gates, Oprah Winfrey, Michael Jordan, Aliko Dangote na wengine wengi. Huko tunakutana na mawazo yao na jinsi walivyo fikia mafaniko waliyo nayo sasa.
Vitabu ni suluhisho la matatizo mengi?
" kama unaishi endelea kujifunza namna ya kuishi'' alisema Seneca. Ni katika vitabu tunakuta suluhu za matatizo mengi. Vitabu vinatoa namna ya kugundua kipaji, kuishi na watu, kutengeneza pesa na kuwa kiongozi. Hivyo tujifunze kusoma vitabu ili tupate fumbuzi za matatizo mbalimbali.
Vitabu vinabadili maisha.
Mwandishi wa kitabu cha "Who will cry" Bwana Tony Robbins anasema " mtu ambaye utakuwa miaka mitano toka sasa atatokea katika vishawishi viwili, watu unaoishi nao/kushirikiana nao na vitabu unavyosoma. Tujifunze kumbe kuweka bidii katika kusoma.

Wataalamu wanasema kila siku kila mtu inabidi achukue dakika kumi na tano akisoma kitabu aijalishi amebanwa kiasi gani, akifanya ivo atasoma vitabu viwili kwa wiki,20 kwa mwezi na vitabu 1000 kwa mwaka mzima. Kumbe kila siku iitwayo Leo tujitahidi kusoma vitabu. Mimi binafsi kila asubuhi baada ya kuamka na kusali lazima nisome kitabu kimojawapo. Na vitabu vimenibadilisha mpaka sasa mambo mengi ninayoweza kuwashirikisha kutoka kweny blog yangu ni mawazo ya vitabu.
Kama utahitaji vitabu mbalimbali tuwasiliane kwenye namba ntakazo weka hapo chini ili uwezo kuvipata na wewe ubadili maisha yako. Uanze mwaka mpya kwa mitazamo mipya.
Ni mimi rafiki na ndugu yenu.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiane;
0764145476
Whatsapp: 0625951842 (tuma neno SUBSCRIBE niwe nakutumia makala zangu)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Edius Bide Katamugora
Tuwasiane;
0764145476
Whatsapp: 0625951842 (tuma neno SUBSCRIBE niwe nakutumia makala zangu)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Usisahau kulike page ya Facebook @bideismblog
Endelea kusoma makala nzuri toka blog hii.
" See you at the top".
0 comments:
Post a Comment