Tuesday 8 November 2016

Kuamua Lini Uanze Ni Adui Wa Kuanza.

Habari mpendwa msomaji wa Bideism blog. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na kutafuta maisha yenye mafanikio.

"Deciding when to start is the enemy of starting". Kuamua lini uanze ni adui wa kuanza. Ni mara ngapi tumekuwa tukipanga mambo mengi tuyafanye lakini tunashindwa?. Januari wakati mwaka umeanza uliweka mipango mingi tu utakayo ifanya mwaka mzima. Je umetimiza mipango yako au ndo bado umesubiri mwezi mmoja uliobaki uanze?.

Wapendwa unapohamua kufanya jambo Fulani usianze kuwaza utalifanyaje, tumia kidogo ulichonacho. Kampuni ya Cocacola wakati inaanza kutengeneza vinywaji iliuza chupa 25 tu kwa mwaka mzima!!!!. Usishangae hawakuchoka kufanya mambo waliyoyapanga. Leo hii nani asiyeifahamu cocacola duniani?.

Katika kuanza kitu au jambo Fulani changamoto utakutana Nazo tu. Njia ya mafanikio haijanyooka. Changamoto ni kama mtihani anaotoa mwalimu ili mwanafunzi afaulu. Usikate tamaa hakikisha unafaulu mtihani wa changamoto.

Kuna bwana mmoja alikuwa anachimba madini sehemu lakini hakufanikiwa akaamua kuacha akamuuzia MTU mwingine, mtu Huyo alikuja na kuanza kuchimba ardhi, umbali wa mita moja alikuta bahari ya madini. Kumbe tunapoamua kuanza jambo Fulani tujitoe kwa moyo mmoja na tusiwe watu wa kusitasita. Wahenga wanasema "Chelewa chelewa utakuta mwana si wako". Na mlango wa fursa hauna alama za vuta/sukuma.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako Eddy Bide.
Tuwasiliane: 0764145476.
Whatsapp; 0625951842.
Email: ekatamugora@gmail.com @

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: