Wednesday, 16 August 2017

Adui Wa Nje Na Adui Wa Ndani

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya na umeamka salama. Tumshukuru Mungu kwa kutupatia siku nzuri kama ya Leo.
Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandalia ili uweze kujifunza kitu kipya kitakachokusaidia.

Leo hii tutafakari kidogo kuhusu adui wa nje na adui wa ndani. Ninaposema adui najua unanielewa vizuri. Huyu ni mtu ambaye unakuwa naye katika uhasama. Inafikia hatua ukiona anakuja njia unayotembea wewe unaona ni bora hubadili njia na kupita njia nyingine ili mradi tu usikutane naye wala kumuona.

Adui niliyemuongelea hapo juu huyu tunamuita adui wa nje. Yaani adui tunayemuona. Ukisikia mtu anakwambia mtu Fulani ni adui wangu, tambua kwamba anaongelea maadui wa nje.

Watu wengi wamekuwa wakisikika wakisema, asingekuwa mtu Fulani jambo Fulani lisingetokea, yeye ndiye aliyenifanya Leo niwe hivi. Namchukia sana mtu yule amenikwamisha. Hawa wanaweza kuwa: mzazi, wazazi, ndugu, rafiki wa karibu, mtu uliyekuwa naye kwenye mahusiano kutaja wachache.

Tubadili shilingi kidogo na kuwaona maadui wa ndani. Huyu ni yule uliyenaye wewe. Adui unayetembea nae. Najua utastuka kusikia hivyo ipo hivyo.

Adui wa ndani ni nani?
Adui wa ndani ni hile sauti unayoisikia ndani yako ikisema "Haiwezekani." "Edius huwezi kufanya kitu Fulani." "(Weka jina lako) huwezi kufanikiwa." Huyu ndiye adui wa ndani. Rafiki yangu naomba nikwambia hakuna adui mbaya kama adui wa ndani. Bora uwe na adui wa nje kumi kuliko kuwa na adui wa ndani mmoja. Kitu kilichowafanya wengi washindwe kutimiza ndoto na malengo yao ni maadui wa ndani wala si maadui wa nje.
Ukiweza kumshinda adui wa ndani adui wa nje hawezi kukuletea madhara yoyote. Kuna methali moja ya kiafrika inasema " Kama hauna adui wa ndani, adui wa nje hawezi kukuletea madhara yoyote. "

Leo hakikisha unapambana na maadui wa ndani. Usianze kusumbukia maadui wa nje wakati wewe akili yako imembeba adui mkubwa ambaye kila mara anakwambia "huwezi kufanikiwa." Wahenga wanasema "fimbo iliyo mkononi ndiyo iuayo nyoka." Kumbe uwezo wa kupambana na adui wa ndani unao wewe. Pingana na adui wa ndani. Usiisikilize ile sauti inayokwambia hauwezi.

"Mafanikio yapo mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya Facebook hapa chini.

Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na rafiki yako kile ulichojifunza.

Kitabu cha Barabara Ya Mafanikio Bado Kinapatikana. Bei 6000/=

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: