Tuesday, 15 August 2017

Ushauri Wa Robert Kiyosaki Na Brian Tracy Kwa Vijana

Robert Kiyosaki ni mmoja wa waandishi mashuhuri na mmoja kati ya watu waliobobea katika mambo yanayohusu biashara na elimu kuhusu pesa. Ameandika kitabu kilichouza kopi zaidi ya milioni moja dunia nzima na ndicho kitabu kinachopendwa na wengi. Kitabu hicho alikiita "Rich Dad, Poor Dad." Yaani "Baba Tajiri na Baba Maskini." Ambapo anaelezea kuwa yeye alikuwa na baba wawili mmoja tajiri na mwingine maskini.

Baba maskini ndiye baba yake mzazi. Na baba tajiri alikuwa rafiki wa baba yake lakini ndiye aliyemfundisha mambo mengi hadi Leo hii amekuwa mshauri wa watu wengi duniani nikiwemo Mimi. Kiyosaki ameandika vitabu vingi pia vinavyohusu, ujasiriamali na elimu na biashara.

Ushauri wake kwa Vijana;
1) Fanya kazi bure:
Najua utashangaa hili tena wasomi wengi ndio watu ambao ukiwaambia kuhusu kazi fulani watakuuliza "wanalipa kiasi gani?" Lakini ushauri wake, ni kwamba unapotaka kufanya kazi kwanza anza kwa kufanya bure, jitolee. Kuna watu wengi walianza kazi kwa kujitolea na hatimaye wameajiriwa katika kampuni hizo walizokuwa wakijitolea na kupewa vyeo vikubwa tu.
Robert kiyosaki yeye alikuwa akifanya kazi bure kwa rafiki ya baba yake bila kupata malipo yoyote.

2) Kua ukiwa unajifunza (grow to learn);
Ukiwa kijana, unahitaji kujifunza mambo mengi. Kama nilivyosema, ukifanya kazi bure jifunze mambo mengi kadri uwezavyo. Jifunze kila kitu. Robert Kiyosaki anasema mfano wa mtu yeyote anayefanya kazi kwenye mgahawa wa McDonald anaweza kuanzisha kampuni kubwa na kufanya biashara yake kuwa ya kimataifa. McDonald ni sehemu nzuri ya kujifunza kuwa kiongozi yeyote wa kampuni hata ukiwa muhudumu au mpishi. Huhitaji kwenda McDonald ndipo ujifunze kila mahali unaweza kujifunza, linalofanyika Marekani, linaweza kufanya Afrika, tafuta Leo ofisi au sehemu ya kujitolea nenda jifunze kufanya kila kazi, usichague wa kubagua kazi.

Brian Tracy:
Huyu ameandika vitabu vingi vya maendeleo binafsi, uhamasishaji na ujasiriamali. Ni moja kati ya waandishi maarufu duniani. Na amekuwa mshauri wa serikali nyingi duniani. Analiwahi kusema kwamba alisoma vitabu zaidi ya 700 ndani ya mwaka mmoja.

Ushauri wake kwa Vijana:

1) Unapopata kazi mwambie bosi hupo tayari kufanya kazi nyingi;
Mwambie bosi wake, umekuja kwenye kampuni yake kuiletea maendeleo na mafanikio makubwa. Muombe akupe kazi nyingi kadri awezavyo. Ukiwa mtu wa namna hiyo, utakuwa wa tofauti na utakuwa mtu wa manufaa na kampuni lazima itakuthamini.

2) Ukipewa kazi jitahidi iishe kabla ya wakati tarajiwa;
Hata kama ukipewa majukumu mengi kiasi gani yafanye haraka na kwa weledi mkubwa uwezavyo. Kama ni kazi ya wiki moja wewe tumia siku nne kuikamilisha. Ukifanya hivyo utapata mafanikio makubwa.

Hebu tukikumbushe mambo muhimu ymtuliyojifunza
1) Jitolee na Fanya kazi bure kila mara unapopata nafasi.

2) Jifunze kadri uwezavyo namna ya kufanya kazi. Jifunze mambo tofauti tofauti, ikiwezekana mambo yote yanayohusiana na kazi yako.

3) Omba kupewa kazi nyingi

4) Unapopewa kazi hata ziwe nyingi vipi, jitahidi kuzikamilisha kwa muda mfupi kadri uwezavyo.

Nakutakia utekelezaji mwema.

"Mafanikio yapo mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Author and Motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya Facebook hapa chini.

Imani yangu ni kwamba, mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na rafiki yako kile ulichojifunza.

Karibu kujipatia kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio bei 6000/= Tunatuma popote mikoani.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: