Wakati mwaka 2016 unakaribia au umeisha ulijiwekea malengo mengi ya kutimiza mwaka huu wa 2017.
Tena wengine wakaenda mbali na kuyaandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu na malengo.
Swali langu kubwa kwako Leo ni Je bado unatimiza malengo yako?
Jibu au majibu unayowewe na nafsi yako.
Jukumu langu Mimi Leo ni kukumbusha tu kuendelea kutimiza yale malengo uliyoyaweka mwaka Jana.
Jukumu langu Mimi Leo ni kukumbusha tu kuendelea kutimiza yale malengo uliyoyaweka mwaka Jana.
Uchunguzi unaonesha kwamba malengo mengi hufa ifikapo wiki ya pili ya mwezi Februari. Yaani mwaka unapoanza watu wengi wanakuwa na hamasa ya kutimiza malengo yao lakini baadae hamasa hile waliyokuwa nayo inakufa na wanaacha kutimiza na kuendelea malengo yao.
Kama na wewe ulijiwekea malengo ya kutimiza mwaka huu lakini umeacha kuyafanyia kazi nakushauri tu uanze kuyafanyia kazi mara moja. Leo zimebaki siku 223, kati ya siku 365. Kumbe bado muda wa kufanya mambo makubwa hupo. Muda wa kutimiza malengo yako bado hupo. Amka Leo, yale malengo uliyoyaweka mwaka huu hakikisha yanafanyika kama ulivyoyataka yafanyike.
Kama malengo yako uliyaandika mahali Fulani. Chukua kitabu chako anza kuyasoma upya. Yasome kila ukiamka na kabla ya kulala. Ikiwezekana yabandike mahali panapoonekana ili uyaone kila siku yazidi kukupa hamasa ya kuyatimiza.
Nakutakia utekelezaji mwema.
"Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com
Usisahau kulike page yetu ya Facebook hapa chini.
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na rafiki yako kile ulichojifunza.
Kitabu cha Barabara Ya Mafanikio Bado Kinapatikana. Bei 6000/=
0 comments:
Post a Comment