Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Tumshukuru Mungu kutujalia siku nzuri kama ya Leo. Leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako, usikubali ipotee.
One day can make you grow.
One day can make you grow.
Karibu sana katika makala nzuri ya Leo niliyokuandalia.
Leo kwa jicho la pekee ningependa ujifunze kitu Fulani kutoka kwenye mhanzi wa Kichina (The Chinese Bamboo Tree). Huu ni mmea kama mimea mingine ya kawaida. Kama ulivyojifunza darasa la tatu, ili mmea ukue unahitaji vitu vitatu, ambavyo ni hewa, mwanga na maji. Mhanzi huu pia huhitaji vitu hivyo ili uweze kukua na kupata uhai wake maradafu.
Lakini jambo linaloshangaza katika ukuaji wa mmea huu ni kwamba, mmea huo haukui kama mimea mingine ya kawaida, ukuaji wake sio, kama wa mchicha, mpaini, muhindi, mparachichi, mkorosho, mbuyu, au mmea mwingine unaoufahamu wewe.
Katika mwaka wa kwanza mbegu ya mhanzi wa kichina inapokuwa ardhini hakuna kitu chochote kinachojitokeza juu ya ardhi.
Mwaka wa pili, hakuna kitu chochote kinachojitokeza juu ya ardhi, wala kuchipua.
Mwaka wa tatu, hakuna kitu chochote kinachojitokeza juu ya ardhi, wala kuchipua.
Mwaka wa nne, hakuna kitu chochote kinachojitokeza juu ya ardhi wala hata kuonesha juu ya ardhi dalili zozote za kuchipua.
Mwaka wa tano, hapa ndipo maajabu mengi utokea. Mbegu ya mhanzi wa kichini hujitokeza juu ya ardhi, au kwa lugha rahisi naweza kusema, huota ardhi inapofika mwaka wa tano.
Kumbuka nimesema mwaka huu wa tano ni wa ajabu sana kwenye ukuaji wa mhanzi wa kichina, kwani Mara tu baada ya kuchipua toka ardhi, ndani ya miezi sita mmea huu hukua na kurefuka urefu wa futi 80 ambazo ni sawa na mita 24.3840 toka ardhini.
Je mhanzi huo hurefuka ni kweli mmea huu hurefuka ndani ya miezi 6 kufikia mita 24 na uchafu?
Jibu ni hapana tena HAPANA kubwa. Ukweli ni kwamba mhanzi huo huanza kurefuka toka mwaka wa kwanza ukiwa bado chini ya ardhi, maana katika mwaka wa tatu mmea huo, usingelipata maji, usingeliweza kukua na kuchipua au kurefuka kufikia usawa huo.
Tujifunze nini kutoka kwenye mhanzi wa kichina?
Najua hadi umeujua tayari mmea huu kuna kitu umejifunza au umekipata lakini ngoja na Mimi nikuongezee ya kwangu.
1. Uvumilivu;
Tunahitaji uvumilivu mkubwa katika Yale mambo tunayoyafanya. Unaweza kuwa unaweka nguvu nyingi lakini huoni matokeo yoyote chanya. Hebu ona mhanzi wa kichina unavyovumilia miaka mitano bila kuonesha ishara yoyote. Unapotaka kukata tamaa na kuacha kile unachokifanya hebu rafiki yangu jaribu kukumbuka maisha ya mmea huu. Waingereza wanasema "Even Rome was not built in a day." Wakimaanisha "Hata Roma, haikujengwa kwa siku moja."

Unaweza kuona ni kwa namna gani uvumilivu umewasaidia wengi kufanya makubwa. Thomas Edson aliweza kufanya majaribio zaidi ya elfu moja ndipo alipoweza kugundua taa inayowaka.
2. Imani(Faith);
Unahitaji kuwa na imani na kile kitu unachokifanya wewe. Watu wengi wanaweza kuja kukukatisha tamaa na kusema jambo Fulani aliwezekani, imani yako itakusukuma na kusema inawezekana. Michael Jordan akiwa shuleni alifukuzwa kwenye timu ya mpira wa kikapu na kuambiwa hawezi lolote. Lakini yeye alikoma na kufanya mazoezi bila kusita. Kilichotokea baada ya hapo ni historia. Yeye amekuwa miongoni mwa wachezaji mpira wa kikapu waliowahi kutokea duniani.

3. Usugu (persistence):
Hii ni hali ya kukomaa na kitu hata kama huoni mwanga mbele yako unaona giza. Kama unajiamini na kwamba jambo unalolifanya litaleta matokeo chanya baadae unahitaji sana usugu na kukomaa nalo mpaka kieleweke. Mbegu ya mhanzi wa kichina kukaa ardhini miaka mitano sio hali ya kawaida ni usugu usio na kifani. Rafiki yangu na wewe komaa ipo siku tu utaboa hapo ulipo, usichoke. Endelea kupambana. "Usiichoke safari" kama asemavyo rafiki yangu Raymond Mgeni. Kumbuka "Pancha sio mwisho wa safari."

"Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi,
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842 (WHATSAPP)
Email: ekatamugora@gmail.com
0625951842 (WHATSAPP)
Email: ekatamugora@gmail.com
Usisahau kulike page yetu ya Facebook hapa chini.
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na rafiki yako kile ulichojifunza.
Usisahau kujipatia nakala ya kitabu changu kizuri cha BARABARA YA MAFANIKIO.
0 comments:
Post a Comment