Habari za aubuhi mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa afya na umeamka salama. Ni jambo jema kumshukuru Mungu kutupatia siku nzuri kama ya Leo.Leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako, usikubali ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana katika Makala niliyokuandalia ili ujifunze kitu kipya.
Kuna vitu vingi sana ambavyo shule haifundishi na haitawahi kukufundisha lakini kwenye maisha ya kila siku ni vitu ambavyo vinawasaidia wengi kutoka hatua moja ya maisha kwenda hatua nyingine.
Moja wapo kati ya vitu ambavyo shule haifundishi na haitawahi kufundisha ni ushirikiano. Kwanza kabisa mfumo wa elimu karibia dunia mzima ni mfumo ambao unakandamiza kuwepo ushirikiano baina ya mwanafunzi na mwanafunzi.
Kwenye mitihani mnapangwa misitari iliyonyooka tena wakati mwingine nafasi zinaachwa baina ya mtu na mtu, mapolisi na migambo wanaletwa ili kuhakikisha hakuna kitu chochote kinachojitokeza. Hapa namaanisha shuleni ukijifanya una ushirikiano ndicho kitu kinachoitwa kuibia (cheating). Ukikamatwa tu unaibia tayari umefeli mtihani. Kwa vyuoni unadisko.
Lakini kwenye maisha ya kila siku ushirikiano ni kitu muhimu kinachowasaidia watu wengi kuliko kawaida. Kama ni mfanyabiashara atashirikiana na watu wengine, wafanyakazi hivyo hivyo, ushirikiano huleta umoja na kukamilisha msemo unaosema "Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu."
Wasomi wengi wanashindwa sana kuendelea kimaisha kwa sababu tu wanachukua yale waliyoyabeba shuleni na kwenda nayo mtaani. Yaani hule uchoyo aliofundishwa kwenye mtihani anaubeba na kuupeleka kwenye maisha ya kila siku. Hapo ndipo wasomi wengi wanaanzia kufeli.
Rafiki yangu unahitaji kutambua kwamba watu wengi waliofanikiwa wanashirikiana na watu wengine ili kuleta mabadiliko na kufanikiwa. Mwaka 1998, Jack Ma alikutana na wenzake 18, na kuanzisha kampuni ya Alibaba ambayo hakuwa na mtaji wa kuwekeza lakini wenzake walimsaidia kutimiza wazo lake la kutumia intaneti kuuza bidhaa mbalimbali kote duniani. Jack Ma ambaye alizaliwa katika familia duni na maskini ambaye alikataliwa mara nyingi alipoomba kazi mbalimbali Leo hii ni Bilionea na sio bilionea tu Bali ni tajiri namba moja nchini China.
Nimekupa maisha mafupi ya Alibaba ili uone jinsi ushirikiano unavyofanya kazi na ulivyo na nguvu kubwa.
Kumbe rafiki yangu kuanzia Leo tena sasa hivi jenga tabia ya kushirikiana na wenzako. Tafuta siku zote watu wenye ujuzi zaidi yako na hujitahidi kuwafanya marafiki zako na ushirikiane nao. Kama bado unasoma njia nzuri ya kukuza ushirikiano baina yako na wanafunzi wenzako ni kuanzisha kundi la kufanya discussion ambayo itawajengea moyo wa kufanya mambo kwa pamoja.
Makampuni makubwa unayoyaona kila kukicha yanafanikiwa ni makampuni ambayo ushirikiano unabeba nguzo kubwa katika utendaji kazi wao.
Kuna msemo unasema "Vichwa viwili ni zaidi ya kimoja." Kumbe ukiwa tayari kufanya kazi na wenzako kwa ushirikiano mambo mengi ambayo kwako ni magumu yanaweza kuwa rahisi.
Nimegundua kitu kikubwa katika ushirikiano.
Ndiyo maana nimeamua kukupa siri hii uweze kuitumia.
Ndiyo maana nimeamua kukupa siri hii uweze kuitumia.
Kumbuka, hakikisha mara nyingi unatafuta watu wenye uwezo mkubwa zaidi yako. Mwalimu wangu wa hesabu kidato cha sita alizoea kusema "Usijifunze hesabu na vilaza, utakuwa kilaza pia."
Sina maana kwamba wenye uwezo mdogo watengwe la hasha. Lakini wao pia wanaweza kujifunza na kuwa na uwezo mkubwa. Hipo wazi kwamba kila mtu amezaliwa mshindi.
Nakutakia ushirikiano mwema rafiki yangu.
"Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi,
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842 (WHATSAPP)
Email: ekatamugora@gmail.com
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842 (WHATSAPP)
Email: ekatamugora@gmail.com
Usisahau kulike page yetu ya Facebook hapa chini.
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na rafiki yako kile ulichojifunza.
Usisahau kujipatia nakala ya kitabu changu kizuri cha BARABARA YA MAFANIKIO.
0 comments:
Post a Comment