"Ukitaka mambo yaende kama unavyotaka lazima ufanye mambo kwa ufanisi wa hali ya juu sana." Edius Katamugora
Kama kuna kitu ambacho watu wengi hatukijui kinachosaidia kuleta uzalishaji wa hali ya juu ni umoja na kupatana.
Unahitaji kupatana na kuwa na umoja na watu wengine ili uweze kupata kile unachokihitaji.
Kila mtu aliyefanikiwa amesaidiwa na watu wengine na sio kwamba amefika mahali hapo peke yake. Makampuni makubwa unayoyaona yameendelea si kwa sababu ya kuwa na watu matajiri au viongozi wenye pesa bali wana wafanyakazi ambao wanapata na kufanya kazi kwa bidii na umoja.
Ukitaka kufanya kitu ambacho kitakuletea matokeo mazuri sana hakikisha umeongana na unashirikiana na watu wengine. Ukitaka kufanya mambo peke yako kushindwa kwako litakuwa ni jambo La kugusa. Kuna msemo unasema "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu."
Bofya hapa kusoma; Kitu ambacho hukujifunza Shuleni.
Ngoja nikuoneshe kwa mifano:
Kampuni ya Microsoft ilianzishwa na Bill Gates na Paul Allen. YouTube inamilikiwa na watu watatu: Chad Hurley, Steven Chen na Juwed Karim ambapo walianzisha mtandao huo wa kijamii mwaka 2005. Facebook ilianzishwa na watu wanne ingawa Mark Zuckerberg ndiye anayetajwa lakini aliianzisha akiwa pamoja na wanadarasa wake; Dustin Muskovitz, Eduardo Saverin na Chris Hughos. Kampuni ya Tecno hakuinzisha Nnamdi Egeizbo peke yake bali alikuwa na mchina ndiye waliyeanza wote kutengeneza simu.
Kampuni ya Alibaba ilianzishwa na watu 18, ingawa Jack Ma ndiye anayetajwa kama mmiliki. WhatsApp haikuanzishwa na Brian Acton peke yake bali alikuwa na Jan Koum.

Kumbe mafanikio makubwa yatakuja kwa jinsi na kadri unavyoshirikiana na watu wengine.
Mapatano na ushirika ni jambo kubwa katika maisha ya mwanadamu. Kama taifa likitaka kuendelea na kustawi ni lazima watu wake washirikiane na kupatana. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
Tukitupa macho yetu kila kona tutaweza kuthibitisha ukweli wa maneno haya:
Siafu peke yake hawezi kufanya kitu, wala nyuki, wala sisimozi; lakini jumla ya siafu au nyuki au sisimizi wakipatana na kushirikiana katika tendo, basi wanaweza kufanya ajabu kabisa.
Siafu peke yake hawezi kufanya kitu, wala nyuki, wala sisimozi; lakini jumla ya siafu au nyuki au sisimizi wakipatana na kushirikiana katika tendo, basi wanaweza kufanya ajabu kabisa.
Siafu wanaweza kujenga njia na kushambulia wadudu wengine; nyuki wanaweza kutengeneza habari zote za ajabu za mzinga; sisimizi wanaweza kula mdudu mkubwa.
Kwa maelezo madogo ya viumbe au wadudu wadogo hapo juu ambao wakiungana wanafanya maajabu makubwa basi kumbe hata binadamu wakiungana wanaweza kufanya kitu kwa uhodari na ufanisi wa hali ya juu sana.
Ni dhahiri ya kwamba mtu akikaa peke yake au kufanya mambo peke yake bila kushirikiana na wengine watakaa katika hali ile ile waliyonayo wala hawaendelei hata kidogo. Lakini mara wakianza kuungana na kushirikiana na wenzao, basi hapo wote hupata faida; maana watu hufundishwa mambo mapya wasiyoyajua, na husaidiwa na nguvu za wenzao.
Uzi mmoja hauna nguvu nyingi, lakini nyuzi nyingi zikisokotwa, hufanya kwamba yenye nguvu inayoweza kufunga tembo asiweze kujijongeza.
Kumbe ukitaka kufanya kitu kitakachokuletea mafanikio ya haraka sana anza kushirikiana na wenzako. Lakini kumbuka kushirikiana na watu sahihi, ajiri watu sahihi, Fanya kazi na watu sahihi. Nakubaliana na Zig Ziglar aliyewahi kusema "Utapata kile unachokitafuta endapo utawasaidia wenzako kupata wanachokitafuta."
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapatikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842
Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza
0 comments:
Post a Comment