Saturday, 2 September 2017

Vitu Vinavyoweza Kukutoa Kwenye Usaili Kabla Ya Kufika Kwenye Usaili.

Wakati dunia inabadilika kwa spidi ya ajabu sana kumekuwa na mambo ambayo pia yanabadilika kila kukicha.

Kuna watu wengi wamekuwa wakitafuta ajira kila kukicha lakini hawapati. Wamezunguka huku na kule lakini wapi.

Bofya hapa kusoma: Mwanachuo fikiria nje ya box

Wasomi nao wameongezeka jambo linalopelekea vijana wengi kukosa ajira. Takwimu zinaonesha kwamba kila mwaka wanahitimu watu milioni mbili lakini wanaongia kwenye soko la ajira ni laki mbili tu.
Sasa kama umeacha kufikiri nje ya ajira utafanyaje wakati mambo yanabadilika. Hata namna ya kufanya usaili(interview) imebadilika kutokana na mabadiliko yanayotokea duniani kila siku.


Siku hizi kumekuwa na interview mbili kama ulikuwa hujui. Interview au usaili wa kwanza unafanyika kabla hata haujaingia kwenye chumba cha usaili au haujakutana na wanaokufanyia usaili(interviewees). Na usaili wa pili unafanyika siku ile unapokutana na jopo la watu wakikuuliza maswali kadha wa kadha. Watu wengi wanaifahamu njia ya pili pekee.

Ndiyo maana nakwambia yakwamba kila siku dunia inabadilika na mambo yanabadilika.

Mambo yatakayokukosea ajira kabla hata ya kuingia kwenye usaili; (Aina ya kwanza ya usaili (preinterview))

1) Mawasiliano yako kwenye simu.
Najua utashangaa lakini yanatokea na ninayoyaandika yapo. Kutokana na watu kuwa wengi wanaoomba ajira zimegunduliwa njia za kupunguza baadhi ya watu ambao hata wanaondolewa hawafiki kwenye siku ya usaili.

Kwa kutumia simu mwajiri anaweza kukupigia ili asikie unazungumzaje na watu( how do you communicate?). Watu wengi wameshindwa au wanashindwa kufanya mazungumzo mazuri pale wanapoongea na simu. Hapa mwajiri anaweza kutambua wewe ni mtu wa namna gani kwa kuwasiliana na wewe kwenye simu tu. Jitahidi kuanzia Leo jinsi na namna unavyoongea na mtu kwenye simu uongee kwa ustaharabu na hekima ya hali ya juu. Jitahidi kumuita mtu kaka au dada hata kama ni mdogo wako.

Usipokubali kubadilisha namna unavyofanya mazungumzo yako kwenye simu, interview utazisikia kwa wenzako.

2) Mitandao Ya Kijamii;
Mitandao ya kijamii kama Twitter, Instagram na Facebook inaelezea vizuri wewe ni mtu wa namna gani. Nikifungua kwa mfano Instagram yako picha tatu nitakazo kutana nazo zinaweza kunionesha wewe ni mtu wa namna gani. Usishangae kabla ya usaili unaombwa majina unayotumia kwenye mitandao ya kijamii. Kama unapost mambo ya ajabu ajabu jiandae kuzisikia habari za interview kama askari polisi na treni.

Hakikisha picha unazoziweka kwenye mtandao ni picha zenye busara na za heshima. Kama ni mdada usiweke picha za nusu uchi. Kama ni mkaka acha mambo ya kuvaa suruali zilizochanika, kuvaa mlegezo na kuziweka mtandaoni. Zitakuponza.

Kama ni mitandao ya Twitter na Facebook acha kuweka post za ajabu ajabu. Leo unaweka Bifu la Alikiba na Diamond kesho, Mara uchaguzi Kenya utarudiwa, keshokutwa Wenger out. Wewe si mwandishi wa habari za umbea. Habari zako zitakuponza.


Kumbuka mambo mawili yanaweza kukusababisha kukosa ajira bila hata ya kuingia kwenye usaili:

1) Mawasiliano kwenye simu; hakikisha unatengeneza njia nzuri ya kuwasiliana na watu kwenye simu. Hii ndiyo inatakusaidia kwenye kitu kinachoitwa huduma kwa wateja (customer care). Sio lazima uongee vizuri kwenye simu pekee hata unavyoongea na rafiki zako, ndugu jamaa na marafiki ongea nao kwa heshima.

2) Mitando ya kijamii: acha kuweka picha za ajabu ajabu kwenye mitandao ya kijamii. Acha kuandika maneno ya ajabu kwenye mitandao ya kijamii. Mitandao inaweza kukuelezea kwa undani wewe ni nani hata kama haujakutana na mtu yeyote. Kama ulikuwa unaweka picha za ajabu na maneno(status) za ajabu nakushauri uzifute mara moja maana zitakugharimu siku za mbeleni.

Usikose makala ya kesho mwendelezo wa Makala hii ambapo mambo yanayoweza kukukosesha kazi siku yenyewe ya usaili.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi:
  Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapatikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842

Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: