Juzi tuliona aina ya kwanza ya usaili ambapo tuliona kwamba aina hii ya usaili ufanyika kabla hata haujafika mahali wanakofanyia interview.
Kama ukubahatika kusoma bofya hapa:Vitu vinavyoweza kukutoa kwenye usaili, kabla ya kuingia kwenye usaili
Nashukuru sana maana watu wengi walinipa mrejesho na kusema walilielewa vizuri somo lile.
Basi Leo tumalizie hatua ya pili ya usaili ambayo mtu anakwenda mahali wanakofanyia usaili.
Leo ningependa ufahamu vitu baadhi unavyovihitaji wakati unapotakiwa kuingia kwenye usaili. Kama ukivikosa vitu hivyo ni dhahiri kuwa kupata kwako kazi au kufaulu katika usaili huo itakuwa kazi ngumu:
1) Mavazi yako:
Jinsi unavyovaa na kuonekana siku ya usaili itachangia sana kwako wewe kufaulu usaili au kushindwa. Kama umezoea kuvaa ovyo ovyo sio rahisi kwako kuvalia vizuri siku ya usaili maana mbwa mzee huwezi kumfundisha tabia mpya yaani "You can't teach an old dog new tricks." Anza Leo hii kuvaa mavazi yenye heshima na mazuri.

SOMA: First impression matters
2) Matendo yako ya mwili (Body language): Matendo yako ya mwili yanabeba asilimia 65 ya kukufahamu wewe ni nani. Unachoongea kinabeba asilimia 35 tu. Kumbe watu wanaweza kukuhukumu kutokana na Matendo yako ya mwili. Mfano kuongea umeweka mikono mfukoni inaonesha umekosa hekima na heshima. Pili mtu anayekunja mikono kuelekea kwake anaonekana ni mtu anayejilinda na anayekuja miguu pia kwa lugha rahisi naweza kusema defensive body language.
3) Swali la kwanza utakaloulizwa:
Moja wapi ya swali la msingi utakaloulizwa ni "Twambie kuhusu wewe/ wewe ni nani?" (Tell us about you). Kuna Lindi kubwa la watu hawafahamu wao ni watu wa aina gani. Hapa unatakiwa kufahamu unaujuzi gani na umefanya kazi wapi na wapi. Ndiyo maana utasikia wanahitajika watu wenye uzoefu. Ndiyo maana kila siku nasisitiza vijana wajitolee. Kama uliwahi kujitolea kufanya kazi mahali unaweza kujibu swali la wewe ni nani kwa ukamilifu kabisa.

4) Tizama yako ya macho (eye contact):
Hapa unahitaji kuwatizama moja kwa moja wale wanaokufanyia usaili bila kupepesa macho wakati unajibu au kuulizwa maswali.

5) Unaweza kufanya mazungumzo?:
Watu wengi wanashindwa sana kuzungumza mbele za watu. Na hii inaanzia toka wakiwa shuleni. Walipokuwa wakisikia kuelezea kitu mbele ya wanafunzi (presentation) wenzao kazi yao kubwa ilikuwa kujitahidi wasionekane. Je mtu wa namna hii ataweza kufanya mazungumzo mazuri kwenye usaili?. Kama na wewe una tabia ya kujificha kuzungumza mbele ya umati wa watu hakikisha unaimaliza maana itakukosesha kazi bure. Kila inapotokea kazi ya kuelezea jitokeze mstari wa mbele. Hii itakujengea uzoefu na kukuondolea uoga. Anza hata kwa kujitahidi kuzungumza kwenye vikundi vya watu wadogo kama kikundi chako cha majadiliano (Discussion group).

6) Tabasamu:
Tabasamu ni kitu kidogo lakini kinawashinda wengi. Watu wanaotabasamu wanapendwa sana na ni watoa huduma wazuri tu. Nafikiri umewahi kuona wale wafanyakazi wa benki tabasamu haziwaishagi usoni. Au wale wa vodacom huduma kwa wateja ni watu wenye tabasamu (nafikiri Vodacom watanipa ujiko kwa kuwapigia debe). Kuna msemo wa Kichina unasema "Mtu asiye tabasamu haruhusiwi kufungua duka." Kumbe tabasamu linaponya. Kuna watu wengi unakuta amefungua biashara lakini muda wote amenuna, mara nyingi watu wa namna hii hawapatagi wateja.

Mwajiri wako anahitaji watu wanaotabasamu. Wewe endelea kununa. Usitake nikumbuke hule wimbo wa Afande Zombi "Nununu, unamnunia nani?...."
7) Unafahamu lolote kuhusu mahali unapokwenda kuomba ajira:
Moja ya kosa kubwa ni kwenda kuomba kazi na haujafatilia kwa undani mahali ulipoomba kazi wanajihusisha kwa undani na nini. Mwajiri anapenda kujua watu waliokuwa wanaifatilia kampuni yake, taasisi na kadhalika. Kabla ya kwenda kwenye usaili jitahidi umefahamu pale unapoomba kazi unapafahamu kwa kina haswa.

8) Umesoma kitabu gani?:
Nilipoona kitu hicho nilishangaa sana maana kilikuwa kigeni kwangu. Katika karne hii ya ishirini na moja karne ya taarifa kusoma vitabu ni kitu muhimu sana. Usishangae kuulizwa umesoma kitabu gani ndani ya wiki mbili zilizopita. Sasa kama wewe kitabu chako cha mwisho kusoma ni Ngoswe penzi kitovu cha uzembe kidato cha nne au Vuta N'kuvute kidato cha tano na sita, rafiki yangu kazi umeshakosa. Anza na jenga tabia ya kupenda kusoma Vitabu. Hii itakusaidia kupata taarifa, maarifa na pia kubadili namna yako ya kufikiri. Ukitaka kujua uanze kusoma vitabu gani nitafute nitakusaidia. Mawasiliano yangu 0764145476

Zipo njia nyingi za kukufanyia usaili hadi kuhakikisha wewe ni mtu anayefaa kufanya kazi katika kampuni husika. Mfano wa njia ambayo sijaitaja hapo juu ni njia aliyotumia Henry Ford (Mwanzilishi wa kampuni ya kutengeneza magari aina ya Ford) kuwaingiza watu kazini.
Yeye kabla ya kumpa mtu yeyote kazi alikwenda naye kupata chakula cha mchana. Mtu yule kama aliweka chumvi kwenye chakula kabla ya kukionja hakumpa nafasi ya kazi. Maana anafanya mambo bila kujua matokea. Usishangae siku moja na wewe ukafanyiwa hivyo. Jukumu langu ni kukupa mbinu.
Nimalizie na maneno aliyoyasema Ruge Mutahaba Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group akiwa katika fursa jumamosi ya tarehe 3/9/17 huko Morogoro "Wengi wametuma ujumbe mfupi hapa na kusema Fursa inawagusa wafanyabiashara tu na haitizami kuhusu vijana na soko la ajira.
Kijana anayetafuta ajira lazima aelewe kuwa soko la ajira limebadilika kuna mahitaji mapya na ajipime kama yeye ni Problem Solver au Critical Thinker.

Soko la sasa halitizami umepata alama ngapi linatizama ni kiasi gani unaweza kuwa msaada kwa kampuni.
Lazima vijana wafahamu hilo.
Lazima vijana wafahamu hilo.
Halikadhalika kwa WAMANTA wanaohitaji kutoboa mwamba wanahitaji kuwa na sifa kuu tano na za muhimu:
1. Business law
2. Book keeping
3. Branding
4. Sales
5. Soft skills
2. Book keeping
3. Branding
4. Sales
5. Soft skills
Ni muhimu kama WAMANTA kuzifahamu mbinu hizi ili uweze kutoboa."
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie
kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam,
Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapayikana. Mikoani tunatuma
pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842
Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment