Sunday, 29 October 2017

Watu Wanasema Nini Kuhusu Kitabu Cha Barabara Ya Mafanikio?

Leo hii imetimia rasmi miezi minne baada ya kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kuanza kupatikana sokoni na kufika kwenye mikono ya watu Tanzania nzima.
                
Kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kimeandikwa na mwandishi Edius Katamugora kikiwa na utangulizi ulioandikwa na mwandishi mahiri Lazaro Samwel.


Nimepokea maoni mengi baada ya watu wengi kukisoma na kusema ukweli kimekuwa kitabu pendwa na kitabu kilichobadilisha namna ya utendaji kazi wa watu, matumizi bora ya muda, kuwa na fikra chanya na mengine mengi.

Leo hii nimekuandalia makala ili nikudokezee baadhi ya maneno ya watu waliofanikiwa kukisoma kitabu cha Barabara Ya Mafanikio tangu siku kimeanza kufika mikononi mwa watu hadi leo hii:

"Hongera kwa kazi nzuri. Nimeipenda sana kitabu chako." ~Prof. Elisante O. Gabriel (Katibu mkuu wizara ya habari, utamaduni na michezo.)

"Aisee nimefurahi sana kusoma kazi yako. Hongera sana. Nataka uanze kuandika kwenye magazeti, nitahikikisha unafanya hivyo. Barabara Ya Mafanikio usiwe mwisho. Endelea kuandika." Dr. Fr. Faustin Kamugisha (Mwandishi wa vitabu mbalimbali vikiwemo: Matatizo si tatizo, Matatizo ni daraja. Umevaa miwani gani?. Hatupangi kushindwa, tunashindwa kupanga. Andika jina lako vizuri. Make the most of every opportunity kutaja vichache, Lakini pia ni mwandishi wa makala katika magazeti ya Jamhuri, kiongozi na gazeti mojawapo nchini Kenya.)

"Mojawapo ya vitabu bora tulivyochapa mwaka huu ni kitabu chako. Watu wanakipenda sana wakifika hapa ofisini kwetu lazima wakichukue tu. Wewe ni profesa maana vitu kama hivi wanafanya maprofesa." Mr. Adabert Chenche (Mkurugenzi Vipawa Media Link)

"Kuna mtu amekuta kitabu chako hapa kwangu, baada ya kusoma page 2 akakipenda sana ikabidi nimuuzie. Mimi nitachukua kingine." Joas Yunus (Jyb) (Mwandishi kitabu cha Inuka na makala katika magazeti.)

"Leo nimetumia kanuni ya dakika mbili, imenisaidia sana. Asante kwa kitabu chako." Antia, Mwanza.

"Umri wako mdogo hauendani na yale uliyoyaandika kwenye kitabu. Kitabu chako ni kizuri sana. Nimeanza tangu Leo kuwa na wivu wa Mafanikio." Mr Robert, Bukoba Kagera.

"Kanuni ya 20,40,60 nimeifanya kuwa jina la album yangu." Hamis, Mbeya.

"Kuna rafiki yangu kakuta nasoma kitabu chako, kakipenda kanipokonya kasema hadi amalize kukisoma ndipo atakapokirudisha." Jilen Lugome Dar es Salaam.

"Bro, kitabu chako kimenisaidia sana. Nashukuru sana." Kelvin Mwanza.

"Good work. Nimekisoma likizo hii." Innocent, Mbeya.

"Kwangu Mimi kitabu cha Barabara Ya Mafanikio alichokiandika Edius Katamugora ndicho kitabu bora mwaka huu. Ningemshauri kila mmoja akitafute akisome kabla ya mwaka huu kuisha." Godius Rweyongeza (Mwandishi wa kitabu cha Kutoka sifuri hadi kileleni na mmiliki wa Songambele Blog.)

"Mama yangu amesoma sura 3 za mwanzo, amesifia umemuelimisha kuhusu kujali muda." Paskazia Pascal ~Bukoba Kagera.

"Nitoe pongezi kwa upendo huu na kuona tija la Shairi la Subira Yavuta Heri kuwa katika kitabu cha Mwandishi Edius Katamugora cha Barabara Ya Mafanikio ukurasa wa 26." Raymond Mgeni (Mwandishi wa tenzi na malenga wa ubena na mashairi.)

Kama haujabahatika kusoma kitabu cha Barabara Ya Mafanikio muda bado haujaisha hivyo unaweza kujipatia nakala yako popote ulipo. Mikoani tunakutumia.

Unaweza kuwasiliana nami kupitia 0764145476/ 0625951842 ili ujipatie nakala yako. Kinapatikana kwa bei ya shilingi 6000/= tu. 

Karibu sana mpendwa  ili nawewe ufaidike na ufurahi kama wasomaji walivyojieleza hapo juu.

"Umezaliwa kufanikiwa."

"Mafanikio yako, mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji.
0764145476
0625951842 (WhatsApp).
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

2 comments:

ADERITUS NGIMBWA said...

Hakika kitabu hiki, Sio cha kukosa. Kina mambo makubwa ndani yake.

ADERITUS NGIMBWA said...

Hakika kitabu hiki, Sio cha kukosa. Kina mambo makubwa ndani yake.