Saturday, 30 December 2017

Hiki Ndicho Kitabu Unachopaswa Kukisoma Tunapoanza Mwaka 2018

Mwaka huu umekua mwaka wa pekee sana kwangu ambapo nimeweza kusoma vitabu zaidi ya 30. Hii ni hatua kubwa sana ambayo nimeipiga.

Takwimu zinaonesha kwamba mtu wa kawaida husoma kitabu kimoja hadi kufikia vitabu viwili ndani ya mwaka mzima. Lakini viongozi wa makampuni na watu waliofanikiwa wameweza kusoma vitabu zaidi ya 102 ndani ya mwaka mzima.

Siri mojawapo ya watu waliofanikiwa ni kupenda kujifunza na kusoma vitabu ni njia nzuri ya kupata maarifa kwa haraka sana. Kitu ambacho mtu amejifunza kwa zaidi ya miaka 30 wewe unaweza kujifunza ndani ya wiki moja. Hiyo ni mojawapo ya faida kubwa ya watu wanaosoma vitabu. Ukitaka kuwa mmoja wao anza mwaka Mpya kwa kuanza na tabia hii Mpya ya kupenda kusoma vitabu.

Katika mwaka 2017 unaoisha kesho nimepata fursa ya kusoma kitabu kinachoitwa Tatizo Si Rasilimali Zilizopotea kilichoandikwa na mwandishi Godius Rweyongeza ambaye pia amewahi kuandika kitabu kinachoitwa Kutoka Sifuri Hadi Kileleni.

 

Naweza kusema kwa mwaka 2017 kitabu cha Tatizo Si Rasilimali Zilizotea, Tatizo Ni Rasilimali watu Tunaowapoteza ni kitabu bora kwangu. Kimeandikwa kwa hekima kubwa, na kina maarifa yasiyo ya kawaida.

Faida utakazozipata baada ya kusoma kitabu hicho;

1) Kujijua Wewe Ni Nani
Watu wengi hulalamika kwamba kuna Rasilimali za Nchi zinapotea lakini watu wenyewe ndiyo kwanza wamepotea. Mwandishi anatutaka tutumie nguvu tulizonazo hili kuweza kufanikiwa kwa namna ya juu sana. Nguvu hiyo ni akili. Ni watu wachache ambao wameweza kutumia akili zao kwa hali ya juu sana. Kama kila mtu anayetuzunguka akitumia akili zake kwa hali ya juu sana dunia inaweza kuwa mahali pa furaha. Tatizo watu wengi hawajagundua nguvu hii waliyopewa bure. Binafsi nilishtuka sana niliposoma na kugundua kwamba watu unaowaona ni magwiji wa kutumia akili zao, wanatumia asilimia 10 pekee ya akili zao.

Wakati unanyoosha kidole chako na kuwalalamikia wengine, kumbuka kuna vidole vitatu vinaelekea kwako vikionesha kwamba wewe ndiyo tatizo, wewe ndiye wa kulaumu. Na kidole gumba chako kikielekea mbinguni kuleta ushuhuda kwa Mungu kwamba haujabeba majukumu yako yote. Mwandishi pia anatufundisha namna ya kubeba majukumu yetu yote.

2. Namna ya kuweka Malengo Na Kuyatimiza.
Tafiti zinaonesha kwamba watu wengi huachana na malengo yao ifikapo wiki ya pili ya mwezi Februari. Mwandishi wa Tatizo Si Rasilimali Zilizopotea anaelezea kwa kina namna ya kuweka malengo Na kuweza kuyatimiza. Ndiyo maana nikasema hiki ni kitabu unachopaswa kuanza nacho unapofungua mwaka mpya wa 2018.

3. Namna Ya Kugundua Kipaji Chako.
Mwandishi wa kitabu hiki ni mbobezi wa mambo yanayohusu vipaji Na ni mwanzilishi wa Darasa la mtandaoni linaloitwa WhatsApp Talent School (WTS). Mwandishi anasema "Watu wengi wanakubali kuufaidisha udogo kwa vipaji vyao badala ya kuifurahisha dunia." Akimaanisha kwamba kuna watu wengi wanakufa bila ya kutumia hata chembe ya vipaji vyao. Dr Myles Munroe mhamasishaji maarufu toka Marekani aliwahi kuandika akisema "Sehemu tajiri kuliko zote duniani sio Afrika Kusini ambako kuna machimbo ya dhahabu. Sehemu tajiri ni nje kidogo ya mahali unakoishi. Sehemu tajiri kuliko zote duniani ni Makaburini. Huko utakuta vitabu ambavyo havijawahi kuandikwa, nyimbo ambazo hazijawahi kuimbwa, ndoto ambazo hazijawahi kutimizwa, maono ambayo hayajawahi kufikiwa, malengo ambayo hayajatimizwa." Akitaka kuonesha kwamba watu wengi wanaufaidisha udongo zaidi ya dunia kama mwandishi Godius Rweyongeza anavyoelezea.

  Nimekua nikipokea simu mbalimbali nikiulizwa namna ya mtu anavyoweza kugundua kipaji chake na anavyoweza kujipatia pesa kutumia kipaji hicho, Kitabu hicho ni msaada tosha kwa watu wa namna hiyo.

4. Elimu Ya Pesa na Uwekezaji;
Ni vitabu vichache sana hapa Tanzania vinavyoelezea kwa kina kuhusu pesa. Rafiki yangu kumbuka maisha yetu ya kila siku yanaendeshwa na pesa. Pesa ikikosa ndipo utasikia kila mtu unayekutana naye akisema "Vyuma Vimekaza." Lakini hii imetokana na watu kukosa elimu ya pesa.

Godius Rweyongeza ametuletea grisi ambayo itakata kabisa vinywani mwetu msemo huu uliotapakaa kila mahali. Tatizo sio kwamba pesa hakuna, tatizo ni kwamba hauna elimu inayohusu pesa. Tatizo hili lilianza ukiwa mtoto  pale wazazi wako walipokwambia usipende pesa na umesikia maneno hasi yanayohusu pesa, ukaenda shule ambapo hakuna hata mwalimu mmoja aliyewahi kukufundisha elimu hii muhimu sana. Uliishia tu kujua methali ya "Akiba haiozi."

Muda umefika sasa wa wewe kujifunza elimu inayohusu pesa. Mwandishi pia ameelezea uwekezaji unaotakiwa kuufanya. Chukua muda wako sasa usome kitabu hicho cha Tatizo Si Rasilimali Zilizopotea.

Hayo ni baadhi tu ya mambo utakayojifunza endapo utasoma kitabu hicho ingawa yapo mengi zaidi.

Onyo:! Usikubali kuanza mwaka Mpya bila kuanza kusoma kitabu hiki cha Tatizo Si Rasilimali Zilizopotea.

Ili kupata kitabu hicho wasiliana na Mwandishi Godius Rweyongeza kupitia nambari 0755848391. Au unaweza kuwasiliana nami hapa chini ili niweze kukusaidia kupata kitabu hicho.

 "Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com

Mafanikio ni kitu cha kushirikishana washirikishe na wenzako kile ulichojifunza. 

Jipatie kitabu cha Barabara ya Mafanikio kwa shilingi 6000 tu. Tuwasiliane 0764145476.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: