Habari
mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Nichukue fursa hii kukutakia heri yam waka
mpya lakini pia kukupongeza kuumaliza mwaka 2017 salama. Hongera sana kwa
kuuona mwaka 2018.
Leo
hii wakati tumepata fursa ya kuinza siku ya kwanza ya mwaka mpya, mwaka wenye
siku 365, ni sawa na kupewa kitabu chenye kurasa 365 ambazo hazijaandikwa
lolote. Sisi ndiyo watu wenye mamlaka ya kuandika katika kitabu hicho. Tunaweza
kuamua ziwe kurasa hizo hizo 365 au pungufu. Kiwe kitabu chenye jina zuri au
jina baya. Yote hayo yapo mikononi mwetu.
Leo
hii wakati mwaka unaanza ningependa nikukumbushe mambo machache ambayo
unatakiwa kuyafanya katika mwaka 2018:
Mwaka
2018 ni mwaka ambao unapaswa kumtanguliza Mungu. Mungu ndiye aliyekuumba hivyo
ni jukumu lako kumuomba akuongoze katika kila unalolifanya.
Mwaka
2018 ni mwaka ambao unapaswa kujali na kuutunza muda. “Ukitaka kujua thamani ya
mwaka mmoja mwulize mwanafunzi aliyerudia darasa.” Alisema mtu Fulani. Epuka
vitu vinavyokuibia muda, epuka marafiki wanaokuibia muda, mitandao ya kijamii
na vitu vingine.
Mwaka
2018 ni mwaka unaotakiwa kutafuta maarifa na ujuzi kadri ya uwezo wako wote.
Soma vitabu vingi uwezavyo, soma Makala, fika kwenye semina mbalimbali na
workshops(karakana) mbalimbali.
Mwaka
2018 ni mwaka unaotakiwa kufanya uchaguzi. Chagua ni marafiki gani wa
kuambatana nao. Chagua ni watu gani wa kuambatana nao. Badilisha mzunguko wako.
Kaa pamoja na watu wanokufanya ufikiri Zaidi, usikae na watu wanaokwambia
haiwezekani.
Mwaka
2018 ni mwaka ambao unatakiwa kuamua na kusema kwamba majukumu yote ni yako na
ni jukumu lako kuyabeba, hakuna yeyote wa kumlaumu, kuanzia wazazi, ndugu,
marafiki, serikali ns hata raisi wako. “Usimuombe
Mungu akupunguzie matatizo, bali muombe akupe mabega imara yamkuabeba.” Kama
anavyosema DR. Fr. Faustin Kamugisha.
Mwaka
2018 ni mwaka unaopaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu. Nidhamu kwa watu
wanaokuzunguka, nidhamu katika kazi na shughuli zako, nidhamu katika matumizi
ya muda na nidhamu katika matumizi ya pesa.
Mwaka
2018 ni mwaka unaopaswa kukubali kulipz gharama. Watu wengi wanapenda
kufanikiwa lakini hawapendi kulipa gharama. Kuna kulipa gharama katika matumizi
ya muda, pesa, kutaja machache. Amka kabla wengine hawajaamka, fanya kazi
wengine wakipumzika, lala baada yaw engine kulala.
Mwaka
2018 ni mwaka unaotakiwa kuweka akiba. Wahenga walisema “Akiba haiozi, na kama ikioza
hainuki.” Kila pesa unayoingiza
hakikisha unatenga fungu la kumi kama akiba. Kumbuka kuweka akiba kwanza kabla
ujaanza kutumia pesa uliyoingiza. Watu wengi huanza kutumia pesa na kusema
wataweka akiba, mwisho wa siku hujikuta hawanapesa yoyote mikononi mwao.
Mwaka
2018 ni mwaka unaotakiwa kuwajali na kuwapenda watu. Kuna msemo wa zamani
unasema “Watu watakujali baada ya kujua
wewe unawajali na unawapenda.” Shirikiana na watu. Umoja ni nguvu utengano
ni udhaifu. Wakenya wanamsemo unaosema “Ukitaka
kwenda haraka nenda peke yako. Ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako.” Naye
mhamasishaji Zig Ziglar alikua na haya ya kusema “Utapata kitu chochote unachohitaji kama utawasaidia watu kupata kile
wanachokihitaji.”
NAKUTAKIA MWAKA MPYA WA 2018 WENYE
MAFANIKIO TELE.
“MAFANIKIO YAKO MIKONONI MWAKO.’’
Ndimi
EDIUS KATAMUGORA
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625961842 (Whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu cha BARABARA YA
MAFANIKIO KWA SHILINGI 6000 TU. PIGA 0764145476
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni
kitu cha kushirikishana. Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment