Mojawapo kati ya vitu ninavyojivunia ni kuwa na marafiki wenye tija katika maisha yangu. Marafiki waofanya kila siku nijifunze na kupata maarifa mapya. Marafiki wamenifanya niwe mtu wa kujua mambo mengi ambayo kabla sikuweza kuyafahamu wala kuyatambua.
Mwaka Jana nilipata fursa ya kufahamiana na rafiki yangu
mmoja anayeitwa Avith. Huyu ni rafiki ambaye kusema ukweli amesaidia
kuyabadili maisha yangu kwa kiasi kikubwa, ingawa ni rafiki niliyempata
kwa kuchelewa sana.
Siku moja mwaka Jana 2017, nilipata nafasi ya kumtembelea
nyumbani kwake ili tubadilishane, mawili matatu. Kusema ukweli siku hiyo
ilikuwa kama mwaka mzima kwangu kwani nilijifunza mambo mengi na adimu.
Kitu cha kwanza nilichoshangaa ni kwamba rafiki yangu huyo
anasoma vitabu sana na si vitabu tu bali vitabu vyenye gharama kubwa,
ndipo nikakumbuka msemo wa Zig Ziglar unaosema "Masikini huweka Televisheni kubwa masebuleni kwao wakati matajiri huwa na maktaba kubwa."
Shauku yangu haikuishia hapo nikaenda mbali na kumuuliza,
unawezaje kuwa na vitabu vya bei ya juu namna hii wakati watu wengine
ukiwaambia kitabu cha Barabara Ya Mafanikio ni shilingi 6000 tu wanadai
ni pesa kubwa?. A mania via maneno haya " Eddy, mimi ninaposoma kitabu katika kopi laini(soft copy) na kukipenda lazima nifanye jitihada zozote nikiweke katika mikono yangu. Na ni kwasababu tu napenda kutafuta maarifa."
Kisha akaniambia maneno yafuatayo Biblia imeandikwa maneno
mazuri ambayo kila mtu angeliyafahamu tungeweza kuishi maisha yenye
furaha sana.
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako."(Hosea 4:6)
Baada ya kaka Avith kuniambia maneno hayo alisema " Kumbe
kukosa maarifa unaangamia wewe na kizazi chako chote." Ndiyo maana Dr
Myles Munroe aliwahi kusema "Yote ninayoyajua ni yale yote niliyojifunza."
Kaka Avith hakuishia hapo Bali alinifundisha kitu kimoja ambacho Leo hii mimi nakiita kanuni ya 3×3;
Hii ni kanuni muhimu sana kama unataka kuwa mtu wa kayatafuta na kuyasaka maarifa.
Hii ni kanuni muhimu sana kama unataka kuwa mtu wa kayatafuta na kuyasaka maarifa.
Kanuni ya 3×3 ikoje?
Kama ilivyo kila siku unaweza kulilisha tumbo lako Mara tatu kwa siku, akili yako pia inaitaji kulishwa vitu vitatu tofauti kwa siku kila siku.
Kama ilivyo kila siku unaweza kulilisha tumbo lako Mara tatu kwa siku, akili yako pia inaitaji kulishwa vitu vitatu tofauti kwa siku kila siku.
Mambo ambayo unatakiwa kuilisha akili yako kila siku;
1. Neno la Mungu;
Kila mtu ameumbwa na Mungu hivyo maisha yetu ya kila siku yanapaswa kujitahidi kumtafuta na kumjua Mungu. Huwezi kumjua Mungu kama huwezi kulijua neno lake. Kila siku ya Mungu hakikisha unasoma Biblia au Kurani yako na vitabu vya dini. Hii itakusaidia kuwa na imani thabiti na kuwa mtu asiyeteteleka kama kwani wewe umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Jiulize je ni mara ngapi ya mwisho umefungua Biblia au
Kurani yako na kusoma neno la Mungu?. Kama hujawahi kufanya hivyo
nakuomba ukimaliza kusoma makala hii anza kusoma neno la Mungu mara
moja. "Anza siku yako na Mungu, maliza siku yako na Mungu." Anatuhasa Rick Warren, mchungaji na mwandishi wa vitabu.
2. Soma vitabu vinavyohusu maisha;
Hapa simaanishi vitabu vya stori na udaku, la hasha! Namaanisha vitabu vinavyohusu maendeleo binafsi(self help books), ujasiriamali na biashara, uongozi, kutaja machache. Kila siku hakikisha unasoma kitabu Fulani.

Katika kitabu cha Mbinu 7 za kupata Mafanikio Halisi,
mwandishi Aderitus Ngimbwa ameelezea vizuri faida utakazozipata ukianza
kusoma vitabu hivyo, muda wa kusoma vitabu na mambo mengi sana
nakushauri ukitafute ukisome au tuwasiliane ujue namna ya kukipata.
3. Soma vitabu vinavyohusu fani yako;
Watu wengi ukiwaambia kusoma vitabu hufikiria vitabu vya aina hii tu, lakini wanakosea sana kutosoma aina mbili ya vitabu nilivyovitaja hapo juu. Ili uwe mtu wa tofauti hakikisha unasoma mambo mengi yanayohusu fani yako ili ijiyofautishe. Kila mtu anajua mambo katika fani yake lakini kujua zaidi ni tofauti kubwa na dunia ya Leo inahitaji watu wanaojua mambo kwa weredi wa Hali ya juu sana. Kila unachokisomea wewe kuna maelfu ya watu wanakisomea pia. Ukitaka kuwa wa tofauti anza kusoma vitu zaidi kuhusu fani yako soma vitabu.

Bahati mbaya hadi Leo hii tunao wasomi ambao kwao hawajui
lolote kuhusu vitabu, akipewa madesa(pamphlets) anafikiri ujuzi umeishia
hapo. Kama wewe ni mtu wa namna hiyo umejichimbia kaburi na unajizika
mwenyewe.
Nakubaliana na William O'Brien raisi wa zamani wa shirika la Bima linalojulikana kama Hanover aliyewahi kusema "Ngome kubwa ambayo haijawahi kuvumbuliwa ni nafasi iliyo katikati ya maskio." Akimaanisha watu wengi bado hawajaweza kutumia akili zao vilivyo.
Naomba kila siku hakikisha unameza dozi hii ya 3×3 ili uwe mtu wa tofauti na mtu mwenye maarifa usije ukaangamia.
Baada ya rafiki yangu Mr Raymond Mgeni, kusoma makala haya aliamua kuandika utenzi ufuatao hapa chini;
Kutwa Mara 3, Dozi ya Maarifa
Akili Ni Kama Mwili
Maarifa ifikiri
Mara tatu iwe mbali
Siku uitwe hodari
Maarifa ifikiri
Mara tatu iwe mbali
Siku uitwe hodari
Kwanza vya roho kauli
Maisha viwe vya pili
Vile fani siwe mbali
Kote kote ushamiri
Maisha viwe vya pili
Vile fani siwe mbali
Kote kote ushamiri
Edius mefikiri
Hii tiba kweli nzuri
Kuitwa mtu mahiri
Dozi tatu zifikiri
Hii tiba kweli nzuri
Kuitwa mtu mahiri
Dozi tatu zifikiri
Na Jitu la Miraba 4 2018
Mjumbe Malenga wa Ubena
Edius Bide Katamugora
Mjumbe Malenga wa Ubena
Edius Bide Katamugora
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa." (Hosea 4;6)
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi;
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842 {WhatsApp}
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram; ediuskatamugora
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842 {WhatsApp}
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram; ediuskatamugora
Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza kwani mafanikio ni kitu cha kushirikishana.
0 comments:
Post a Comment