Watu wengi tumekuwa na malengo makubwa lakini hatujawahi kuyaandika chini. Watu wengi tumekuwa na maono na ndoto kubwa lakini hatujawahi kuziweka katika maandishi. Wengine hata kumiliki notibuku ya shilingi 500/= iliyoandikwa mipango na malengo yao hawajawahi kuwa nayo.
Ukiandika malengo na mipango yako ni hatua ya kwanza ya kuanza kuweka malengo yako na kuyaweka katika uhalisia. Kama una malengo na hujawahi kuandika sehemu yeyote bado hayo sio malengo Bali ni matamanio( wishes).
Mambo ya kufanya Leo hii;
1. Chukua kalamu na karatasi.
2. Andika malengo yako na mipango yako.
3. Yaweke sehemu ambayo unaweza kuiona kila siku unapoamka na unapolala.
4. Ukiamka yasome na ukitaka kulala hakikisha unayosoma. (Hii itakupa motisha ya kile unachotaka kukifanya, hata ukisahau maandishi yako yatakukumbusha kuna kitu Fulani unatakiwa kukitimiza Leo hii lakini bado haujakitimiza.

"Yaandike maono haya; yaandike wazi juu ya ubao, anayepitia hapo apate kuyasoma." (Habakuki 2:2)
Nakutakia utekelezaji mwema
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842
0 comments:
Post a Comment