Siku moja mwanasayansi Newton akiwa ameketi chini ya mti wa mwembe aliangukiwa kichwani na embe lililotoka mtini. Baada ya kuliokota embe hilo alianza kujiuliza ni kwanini embe hilo limeanguka kutoka mtini na kushuka chini na wala halikwenda juu. Hiyo ikampelekea kugundua kitu kilichoitwa "Acceleration due to gravity."
Kitu kikubwa tunachopaswa kujifunza maishani na kukitumia kila siku ni "kuanza na kwanini?." Ndiyo maana Newton alipojiuliza kwanini aliweza kugundua Acceleration due to gravity.
Tunapaswa kuwa watu wanaojihoji na kujisemesha, kwanini?. Anza na kwanini. Unapoanzisha urafiki Mpya na mtu jiulize kwanini. Je rafiki yako anakuja kukujenga au kukubomoa.
Unapoamua kuacha kazi na kutafuta kazi nyingine. Je umejiuliza kwanini umeacha kazi hiyo na kwanini unaifuta kazi mpya au umeenda kisa tu umesikia ina mshahara mkubwa lakini nyuma ya pazia hujui lolote.
Unapoamua kuacha kusoma masomo Fulani. Je umejiuliza masomo uliyoyaacha yana madhara gani huko mbeleni. Kumbuka neno "ningejua" huja baada ya safari.
Au ndiyo umeamua kuanzisha mahusiano mapya. Je umejiuliza kwanini umeanzisha mahusiano hayo. Au unataka kujionesha kwa mtu aliyekusaliti au kukuacha kwamba hajakupunguzia lolote. Unajiumiza. Au unataka uonekane mbele za watu yakwamba na wewe huko kwenye mahusiano.
Unataka kufanya biashara Fulani. Je umeanza na kwanini unataka kuifanya biashara hiyo? Je una moyo wa kuifanya biashara hiyo?. Au umesikia kwa watu biashara Fulani inalipa? Na wewe ukakubali kirahisi!!.
Sikuzote jifunze kujiuliza na kuanza kusema kwanini. Ukikutana na mtu anayeanza kufanya mazoezi ya mwili utakuta anafanya bila kuchoka, anafanya kila siku. Huyo ni mtu aliyeanza na kujiuliza kwanini. Chochote ulichopanga kukifanya leo hii jiulize kwanini unakifanya au unataka kukifanya. Je ni cha muhimu kwenye maisha yako? Je ni kitu kinachoongeza tija kwenye maisha yako.
- Watu wanaojiuliza kwanini ni wavumbuzi wakubwa katika dunia hii ni watu waliofanikiwa. Baada ya Nnamdi Egeizbo kuona kwanini watu wanatembea na simu nyingi mkononi za kutumia laini moja alijiuliza kwanini watu watembee na simu nyingi mkononi badala ya kutembea na simu moj yenye laini zaidi ya mbili, ndipo alipoamua kuanza kutengenez simu za dizaini hiyo. Leo hii Nnamdi ni tajiri mkubwa anayemiliki stoo kubwa ya kuuza simu inayoitwa SLOT na kampuni za simu za TECNO NA INFINIX.
- Watu wanojiuliza kwanini hawezi kamwe kukata tamaa. Ni watu waliojipanga toka mwanzo.
- Watu wanaoanza na kwanini ni watu wenye malengo na watu wanotimiza malengo yao. Lionel Messi katika udogo wake alikua akiuza chai iliapate pesa itakayo msaidia kufanya mazoezi ya mpira wa miguu, leo hii dunia nzima inamtambua Messi kwa kipaji chake kikubwa cha kusakata kabumbu.
Kuwa mtu wa kuanza na kwanini. Jifunze kuanza na kwanini.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi;
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
E-mail: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
E-mail: ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio Kwa Shilingi 6000 tu.
0 comments:
Post a Comment