Mara
nyingi nimekuwa nikisikia vijana wengi wakijishauri wao kwa wao na kusema chuo
hakisaidii. Mbona matajiri wengi duniani waliacha chuo na wamefanya makubwa
duniani.
Paul
Allen mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft hakuhitimu chuo.
Bill Gates mwanzilishi wa Microsoft hakuhitimu chuo. Mark Zuckerberg mwanzilishi wa Facebook hakuhitimu chuo.
T
D. Jakes hakuhitimu hata sekondari (highschool).
Joel
Osteen hakuhitimu pia elimu ya sekondari.
Said
Salim Bakhresa mwanzilishi na mmiliki wa makampuni ya Bakhersa Group aliacha
shule ya msingi akiwa na miaka 14.
Na sasa hivi ni watu maarufu na waliofanikiwa sana kiuchumi.
Na sasa hivi ni watu maarufu na waliofanikiwa sana kiuchumi.
Je kama Mimi ningeacha chuo Leo ningekuwa kama wao?
Unaacha
chuo una nini? Hili ni swali ambalo kabla hujaamua kusema unaacha chuo inabidi
ukae chini na kujiuliza.
Wakati
Bill Gates akiwa na umri wa miaka 16 na Paul Allen akiwa na miaka 19 tayari
wakikuwa wamekwisha anzisha Microsoft.
Wakati Mark Zuckerberg anaacha kusoma chuo cha Harvard tayari Facebook
ilikua imeanza kufanya kazi.
Je wewe ukitaka kuacha chuo una nini mkononi?
Je wewe ukitaka kuacha chuo una nini mkononi?
Said
Salim Bakhersa katika miaka ya sabini (1970) alikuwa akifanya biashara ya
mgahawa huko Zanzibar kwa miongo mitatu mfulilizo. Huko nyuma aliwahi kufanya
biashara za mikate, viazi na rambaramba (ice
cream)
Wengi
wamekuwa wakifikiri kwamba akienda kufanya biashara atatoboa maana amesikia watu
wengi wamekuwa matajiri kwa kufanya biashara ili hali hajawahi kuuza hata
ubuyu. Maana yangu ni kusema hajui lolote kuhusu biashara lakini amekazana
elimu haisaidii.
Elimu
haitakusaidia lolote kama utakuwa mtu wa kukaa darasani ukishindana na wenzako
ili upate maksi za juu bila kupata ama kuongeza ujuzi. Ili ni tatizo
linaloyakumba mataifa mengi hapa duniani katika sekta ya elimu. Watu wengi
wanashindania kupata maksi za juu lakini si kupata ujuzi. Kukosa ujuzi ni
kukosa maarifa na kama hauna maarifa utaangamia. "Watu wangu
wanaangamia kwa kukosa maarifa." (Hosea 4:6)
Ukiwa na mawazo ya kuacha chuo hakikisha una kitu mkononi kitakachokupeleka mahali unakokwenda. Watu unaowaona wamefanikiwa kibiashara walianza zamani mno. "Nilijijenga na kuibuka Tajiri namba moja Afrika mwaka 2008 lakini haikutokea usiku mmoja. Ilinichukua miaka 30 kufikia Leo hii. Vijana wa siku hizi wanatamani kuwa kama mimi lakini wanapenda itokee usiku mmoja, hawafanyi kazi. Kujenga biashara yenye mafanikio inakupasa uanze kidogo na uwe na ndoto kubwa. Safari ya ujasiriamali ni mshikamano wa lengo kuu." alisema Aliko Dangote. “Ninaweza kukumbuka wakati nilikuwa shuleni la msingi, ningeenda na kununua makandoni ya masanduku ya pipi na ninaanza kuwauza ili tu kupata pesa. Nilikuwa na nia ya biashara hata wakati huo,” anahitimisha Aliko Dangote.
Ukiwazia
kufanya biashara bila kujua yaliyomo ni sawa na kwenda vitani bila silaha.
Unategemea nini. Lazima upigwe kipigo kama alichopata Goliathi.
Usiwaze
sana kuacha chuo wakati hauna kitu chochote unachokijua. Usiwaze kuacha chuo na
kufanya biashara kama haujawahi kufanya biashara ndogo yoyote hata ya kuuza
visheti, bangili na heleni.
Walioacha
chuo, kuna mambo tayari walikwisha yaweka sawa. Walikwisha iona barabara yao ya
mafanikio. Sikushauri uache chuo kama hauna ujuzi wowote na usiwe tu ujuzi bali
ujuzi wa kipekee utakaoleta utofauti kwa jamii inayokuzunguka, taifa na hata
dunia.
Makala hii ni sehemu ya kitabu cha HOW TO BECOME AN EXPERT WHILE AT SCHOOL. Weka Oda yako kupitia 0758594893.
Mafanikio yako mikononi mwako.
Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0758594893
ekatamugora@gmail.com
Www.bideism.blogspot.com
Mwandishi na Mhamasishaji
0758594893
ekatamugora@gmail.com
Www.bideism.blogspot.com
Washirikishe na wengine maana mafanikio ni kitu cha kushirikishana.
Usisahau kupakua APP ya blog hii mwisho kabisa wa ukurasa huu. Bofya sehemu iliyoandikwa DOWNLOAD OUR APP FOR FREE uweze kupata Application yetu.
0 comments:
Post a Comment