Kila siku nitaendelea
kusisitiza jambo hili, ZAMA ZIMEBADILIKA, MAISHA YAMEBADILIKA. Biashara siku
hizi zinafanywa kitaalamu Zaidi ya ilivyokuwa zamani.
Siku za nyuma nilizungumzia
jinsi mtu anavyoweza kujibranda na kuuza bidhaa zake kupitia mitandao ya
kijamii. Kama kuna mtu alianza kufanyia kazi yale niyoyaandika ni matumaini
yangu anaona matokeo ya tofauti sasa.
Mbali na kutumia mitandao ya
kijamii unahitaji pia kuwa na blogu na tovuti ya biashara yako. Sasa utajiuliza
je! Mbona biashara yangu ni ndogo hivyo sihitaji kuwa na blogu au tovuti. Na
mimi nitakuuliza, “kwani biashara yako itakuwa hivyo hivyo miaka mitano au kumi
ijayo?” kama jibu ni ndiyo basi hauhitaji blogu au tovuti kama jibu lako ni
hapana jua kwamba unahitaji kuwa na blogu au tovuti ili kujitanua kibiashara.
Katika mitandao ya kijamii kuna watu wengi wa kufatilia lakini mtu akitembelea
blogu au tovuti yako anakuwa akikufatila wewe pekee.
Zifuatazo
ni faida za kuwa na blogu au tovuti:
1.
Tovuti au blogu yako ni kama
benki, yaani inafanya kazi masaa 24. Benki huwa zinafungwa lakini ATM sikuzote
hazifungwi zinaendelea kutoa huduma za kifedha. Hivyo hivyo blogu au tovuti
yako itakuwa ikitumika masaa ishirini na nne hata kama haupo kwenye biashara yako
lakini watu wana uwezo wa kuona umeingiza bidhaa gani mpya, bei za
bidhaa, n.k.
2.
Tovuti inakusaidia kuwafikia
watu walio nje ya mahali ulipo na hata dunia nzima. Blogu yangu ya BIDEISM
imekuwa ikisomwa na watu wa mataifa yote. Mtu akiingia google na kutafuta
BIDEISM ananipata moja kwa moja.
3.
Blogu au tovuti itakusaidia
kutangaza bidhaa au huduma zako. Kupitia blogu na tovuti utawavuta wateja waje
kwenye biashara yako kwa njia ya matangazo.
4.
Itakuongezea sifa. Watu
wanapenda kufanya kazi au biashara na watu wanaoonekena wataalamu na wale
wanaowafahamu na kuwazoea. Mtu akizoea blogu au tovuti yako ni rahisi kufanya
kazi na wewe pia ni rahisi kukuamini.
5.
Inatoa sapoti ya kimtandao kwa
wateja wako. Kama mtu anashida na biashara yako anaweza kuingia moja kwa moja
kwenye tovuti yako au blogu na kupata majibu. Hii itakusaidia pia kuokoa muda
wako.
6.
Blogu au tovuti inatoa njia ya
watu uwasiliana na wewe. Kwenye blogu yako utaweka jinsi watu wanavyoweza kuwasiliana na wewe hivyo
utawapa mwanya wa kupata mawasiliano yako kiurahisi.
Je unahitaji gharama kubwa
kutengeneza blogu?
Unaweza
kutengeneza blogu wewe mwenyewe. Njia rahisi ni kutumia mitandao ya Wordpress
na Blogger lakini pia unaweza kumwajiri mtu akutengenezee blogu au tovuti yako
hii ndiyo njia ambayo nakushauri uifuate kwani utapata kutengenezewa tovuti au
blogu nzuri ya biashara yako kutoka kwa wataalamu wa mambo ya kutengeneza blog
na tovuti. Kama utahitaji Blogu au Tovuti ya Biashara yako unaweza kuwasiliana nami kupitia namba hapo chini.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
0758594893
ekatamugora@gmail.com
Usisahau kupakua APPLICATION yetu mwisho kabisa wa ukurasa huu sehemu iliyoandikwa DOWNLOAD OUR APP FOR FREE. Bofya hapo utaipata bure.
Mafanikio ni kitu cha kushirikishana washirikishe na wengine.
0 comments:
Post a Comment