Wednesday, 11 April 2018

Kukatishwa Tamaa Ni Kitu Cha Kawaida

Ukiona unafanya kitu ambacho hakuna mtu anayekuja na kukwambia haiwezekani, wewe ni kichaa au hautafanikiwa jua kwamba unafanya kitu cha kawaida sana.

       

Katika safari ya mafanikio utakutana na watu wanaokatisha tamaa. Jiandae kukabiliana nao. Hakuna malipizi mazuri kwa watu wanaokatisha tamaa kama kufanya kitu wakichosema hakiwezekani kikawezekana.

Kuna watu wamejiajiri ili wawaseme watu wengine. Kuna watu ajira yao kubwa ni kukatisha tamaa. Unapokatishwa tamaa usikubaki kukata tamaa kaza moyo usikubali kabisa kushindwa.

Kila unayemwona amefanikiwa alikatishwa tamaa lakini hakuchukua yale maneno aliyoambiwa ya kukatishwa tamaa. Watu ambao hawakukuamini ipo siku watamwambia kila mtu jinsi wakivyokutana na wewe.

Ukitaka watu wasikuseme. Usiwe yeyote. Usifanye lolote. Watu ambao hawasemwi ni watu waliopumzika makaburini. Kama unaishi watu watakuja kukukatisha tamaa. Kumbe kukatishwa tamaa ni jambo la kawaida lakini kwa wale mashujaa wa kutosikiliza maneno ya kukatishwa tamaa.

Robert Fulton baada ya kutengeneza boti aliamua kuifanyia majaribio. Siku ya kuifanyia majaribio kando ya mtu walijaa mashushu na wakatisha tamaa wakisema haitawaka. Boti ikawaka. Ilipoanza kutembea wakasema haitasimama. Kilochotokea ni nini. Boti iliweza kusimama. Usikubali hata sikumoja kukatishwa tamaa. Watu elfu moja wakisema jambo la kipumbavu bado litabaki kuwa la kipumbavu.

Usisahau kupakua APP ya blog hii mwisho kabisa wa ukurasa huu. Bofya sehemu iliyoandikwa DOWNLOAD OUR APP FOR FREE uweze kupata Application yetu.

Jipatie kitabu cha BARABARA YA MAFANIKIO kwa bei ya shilingi 6000/= watu waliokisoma kila siku wanasema kimebadili maisha yao.

"Mafanikio Yako Mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0758594893
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: