Yafuatayo ni mambo niliyojifunza mwezi Aprili:
1. Tanguliza upendo kila
mahali. Utapata chochote unachokitaka kama utawasaidia kupata kile
wanachohitaji
2. Jifunze kuweka bajeti
ya kutafuta maarifa. Kama unavyotenga bajeti ya chakula, tenga bajeti ya
kutafuta maarifa.
3. Ukiona unashindwa
mahali jua kwamba unakosa maarifa kuhusu hicho. Ukiumwa kichwa unaenda kwa
daktari sababu haujui tatizo la kichwa.
4. Kitu kigumu ukikipa
muda kinakuwa rahisi.
5. Marafiki unaoambatana
nao wana mchango mkubwa katika uchumi wako. Ukichagua wenye fikra za kimaskini
jiandae kuwa maskini.
6. Waache watu
wakuchukulie poa usikubali kujichukulia poa. Ukijishushia thamani jua kwamba
hakuna atakayekuja kupandisha thamani yako.
7. Muda pekee wa kutizama
nyuma ni pale unapotaka kujua ni hatua kiasi gani umepiga.
8. Ukitaka kuwa na
matumizi mazuri ya muda wako weka vipambele. Fanya mambo ya muhimu.
9. Mungu hawezi kukupa
kitu ambacho bado hauwezi kukifanya. Mungu hawezi kukupa mzigo ambao hauwezi
kuubeba.
10.Kile
unachokifanya leo ndicho kitakacho tofautisha maisha yako na ya kesho ya baadae
maana maisha yako ya kesho yanategemea nini unafanya leo.
11.
Unaweza
kumaliza wiki bila kutumia mitandao ya kijamii? Kama jibu ni HAPANA jua kwamba
umekwisha athirika na matumizi ya mitandao. Kuwa na kiasi katika matumizi ya
mitandao ya kijamii.
12.Visingizio
na lawama havitakupeleka popote. Acha kulalamika.
13.
Kamwe
usijilinganishe na mtu mwingine. Kulinganisha kunabagua.
14.Imani
ni kama mswaki, utumie kila siku lakini usitumie wa mtu mwingine.
15.Dunia
imebadilika zama zimebadilika, kama una biashara hakikisha biashara yako ipo
mtandaoni.
16.Fursa
zimejificha katika matatizo. Yatizame matatizo kwa jicho la tatu.
17. Umepewa
mdomo mmoja na maskio mawili. Jifunze kusikiliza zaidi ya kuongea. Lakini pia
jifunze kuwa mtu wa mwisho kuongea.
18.When
you update your statuses and apps remember also to update your brain.
19.Muda
wa kufuatilia maisha yaw engine umekwisha. Anza kufuatilia maisha yako.
20. Ukiona
unaona wivu katika kushangilia maisha yaw engine. Jua kwamba itakuchukua muda
kufanikiwa.
21. Tembea
na notibuku kila mahali unapokwenda. Fanya hii kuwa tabia yako. Unaweza kupata
wazo na usiliandike kisha likapotea. Inawezekana wazo hilo ndilo lingekutoa
kimaisha.
22.
Jifunze
kujitolea katika makampuni makubwa. Huko utapata ujuzi na utaweza KUIBA mbinu
mbalimbali za utendaji kazi zitakazo kusaidia katika maisha na kazi zako za
baadae.
23. Ukijikuta
wewe ndiye mwenye uwezo wa zaidi katika chumba ulichomo. Unahitaji kutafuta
chumba kingine.
24.
Kimjaacho
mtu ndicho kimtokacho. “Garbage in, Garbage out.” Unachoingiza akilini mwako
ndicho unachokitoa.
25.Kuwa
mtu wa watu. Dunia ni mji mdogo. Tengeneza marafiki, achana na maadui.
26.
Vitu
vitatu vya kuweka siri:
a) Hatua yako inayofuata
b) Mahusiano yako
c) Kiwango cha pesa
ulichonacho
27.
Fanya
kazi nzuri na ioneshe kwa watu. (Hapa tumia intaneti.)
28.
Andika
kitabu unachotaka kukisoma. Andika unachokipenda na sio kile unachokijua. Andika
stori unayoipenda sana, andika stori unayotaka kuisoma. Kanuni hii itumie
katika maisha yako na katika kazi yako.
29.
Kama
unashawishiwa na mtu Fulani hakikisha unashawishiwa na watu wengine wa namna
hiyo katika sekta hiyo. Ukishawishiwa na Mbwana Samatta, watu watasema wewe ni
Samatta ajaye, ukishawishiwa na kina Mbwana Samatta wengi, watu watasema wewe
ni origino.
30.
Google
kila kitu. Namaanisha google ndoto zako, matatizo yako. Usiulize swali kabla ya
kuliuliza google. Utapata jibu au utapata swali zuri Zaidi ya lako.
Mafanikio yako mikononi
mwako.
Ndimi:
Edius Katamugora
0758594893
ekatamugora@gmail.com
0 comments:
Post a Comment