Monday, 14 May 2018

UBORA NA UZURI WA UKIFANYACHO

Ukifanya kitu fulani kifanye vizuri na kwa ubora kiasi kwamba watu wakikuona unakifanya waende kuwaambia marafiki zao. Hata mimi nikikuona niende kuwaambia rafiki zangu (Ni kawaida yangu kuwatangaza wanaofanya mambo mazuri na kuwaambia wengine waige kwao).
 
Siri hii ndiyo inayotumiwa na kampuni ya Apple.
Wao wanatengeneza bidhaa nzuri na bora za Iphone na Ipad.

 
Kinachotokea ni nini?
 
Wateja au watumiaji wa bidhaa zao ndio wanaowasaidia kutangaza bidhaa zao.
Kwenye biashara pia unahitaji kuwa na bidhaa bora na nzuri ambayo mtu akitumia akamwambie na mwingine kuhusu bidhaa yako.

Watu wanataka vitu vizuri, watu wanataka vitu bora.
 
Watu wako tayari kuingia gharama kubwa ili wapate vitu vizuri na bora.

Wewe pia ni kama bidhaa, hakikisha unajiweka katika ubora wa hali ya juu. Watu wakitaka mtu wa dizaini yako uwe wa kwanza kusema au kutajwa. Usifanye mambo yako ili mradi tu. Fanya mambo kwa ubora wa hali ya juu.

"Mafanikio yako mikononi mwako."
#KijanaWaMaarifa
 
© Edius Katamugora
Mwandishi & Mhamasishaji
0758594893
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: