_________________________________________
Role models ni watu ambao huwa wanakuhamasisha ili siku moja uje kuwa kama wao. Mara nyingi ukisema mtu fulani ni role model wako, kuna baadhi ya vitu ambavyo mnavifanya vitakuwa vinafanana, hivi vinaweza kuwa vipaji au kazi mnazozifanya.
Kama kuna chaguo bora unaloweza kulifanya Leo hii ni kuwa na Role Models wengi. Imekuwa ni kawaida mtu kuwa na role model mmoja, lakini kuwa na role model mmoja sio kitu kizuri.
Leo hii ukiniuliza nani role model wako kwenye uandishi?, usishangae nikakutajia watu zaidi ya kumi. Au ukiniuliza nani role model wako kwenye Public Speaking, usishangae pia nikikutajia watu zaidi ya watu watano.
Kwanini nasema uwe na Role Models wengi?
Ukiwa na role model mmoja ni rahisi sana kuchukua kila kitu kutoka kwake na kujifanya yeye. Watu wataishia kusema huyu ni fulani ajaye.
Ukiwa na role models wengi utaweza kujifunza mambo mengi tofauti na juu yao unaweza kuja na wazo bora na utaonekana origino.
Kila mtu ana vinasaba (DNA) ya tofauti, huyu anaweza kuwa bora katika jambo Fulani, lakini mwingine asiwe bora, kumbe kuwa na role models wengi ni jambo la kushikilia kwa sasa.
Kuna watu wengi wamejaliwa na vipaji vikubwa sana lakini kutokana na Kuwa na role model mmoja, wamesimama na hawawezi tena kusonga mbele.
Mtu akiimba utasikia anaimba sauti kama ya mtu fulani, na watu wakisikia unaimba kama fulani, sio rahisi kukusikiliza wataenda kwa mtu origino ambaye wewe unajisumbua kumwiga.
Mafanikio yako mikononi mwako.
#KijanaWaMaarifa
© Edius Katamugora
0758594893
ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Www.bideism.blogspot.com
0758594893
ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Www.bideism.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment