Ilikua mida ya saa nne asubuhi mwalimu wa somo la kilatini (Latin language) Fr. Novatus Rugoye (R.I.P) alipoingia darasani akiwa ameshikilia makaratasi mengi. Wote tulijua yakwamba amerudisha karatasi zetu za mitihani kwani siku si nyingi tulikua tumefanya mtihani wa kilatini.
Ulikua mwaka 2009 Februari nikiwa darasa la saba. Mwalimu huyo alijua kuongea kingereza haswa na Leo hii ndiye aliyefanya kingereza changu kiwe hivi.
Basi bwana Karatasi zikaanza kugawiwa kila mtu akipata yake. Shule yetu ilikua na wastani wa kila kipindi hivyo ili ufaulu lazima ufikishe alama 55 kila kipindi. Kwenye kipindi cha kilatini kama usipofikisha 55 ulikua umefeli na ulikua unachezea fimbo zisizohesabika. Fimbo za miguuni.
Karatasi zikagawiwa baadae nikasikia jina 'Edius Katamugora' nikaitika 'Yes Father', nikajongea mbele kwa hofu kubwa kwani nilijua nilichokifanya kwenye mtihani. Mwalimu akaniuliza, "How many marks do you think you have." 'Unafikiri umepata alama ngapi?.'
Sikujibu nilikaa kimya maana nilihisi nimepigwa sindano ya ganzi, gafla nikasiki "Eeeh..... you have zero." "Eeeh... Umepata sifuri." Aisee inawezekana niliwahi kupata maumivu mengi lakini kupata sifuri yalikuwa maumivu makubwa ambayo niliwahi kuyapata.
Siku hiyo nilipigwa fimbo hata sikumbuki idadi. Kwakweli ilinipasa kupigwa fimbo zile. Wenzangu wakaanza kunicheka. Siku hiyo nilitamani niache shule, nilitamani nichimbe shimbo nijifukie nisionekane tena mbele ya wanafunzi wenzangu.
Mungu si Athumani siku zilipita bado nikawa naona zero kama mzigo mzito usiobebeka. Lakini nikasema lazima kuna kitu natakiwa nifanye, wote wanaofaulu wako kama Mimi, wengine niliwahi kusoma nao, wengine najua kuwa nawazidi uwezo, lazima nipambane.
Matokeo yalipotoka ya vipindi vyote kwa ujumla ya mwezi Februari nilikuwa wa kumi (10) nikiwa mtu wa mwisho kufikisha wastani wa shule pamoja na kuwa na sifuri kwenye somo la kilatini.
Matokeo yalikuwa yakibandikwa kwenye notisi bodi ya shule. Siku yalipotoka siku na hamu ya kuyaona kwani sifuri ilikua bado inaniumiza roho. Aisee kupata sifuri ni masononeko makubwa ukiwa shuleni. Siku hiyo akaja kijana mmoja akasema, "Edius wewe ni wa ajabu, umepata zero (sifuri) lakini bado umekuwa wa kumi!" Aisee huyo mtu kama alikuwa malaika aliyetumwa na Mungu kusema nami, nilijiona naweza nikasema kumbe Mimi ni "Genius".
Toka siku hiyo nikaanza kusoma kilatini kwa nguvu zangu zote. Mwezi uliofuata nikapata 35, nikasema " inawezekana." Kutoka sifuri hadi 35 si haba. Ingawa viboko niliendelea kuchezea kwani 55 ilikua haijatimi.
Mwezi Novemba mwaka huo kikatokea kitu cha Historia ambacho ndicho kimebeba stori hii. (Tulipokua tunahitimu la saba, tulikua tunarudi shuleni ili kujiandaa na kidato cha kwanza, (pre-form one))
Ilikua asubuhi mwalimu mmoja akatuita mesini, (Dining Hall) akiwa ameshika karatasi nyeupe. Kumbe ilikua ni karatasi ya matokeo ya mwezi Novemba. Basi akasema anaanza kusoma toka mtu wa kwanza hadi wa mwisho, ukisikia jina lako unasimama unaingia kwenye mstari.
Akasomwa mtu wa kwanza akatoka akasimama. Unajua nini,? Kilichofuata ni historia, nikasikia mtu wa pili, "Edius Katamugora." Aisee siku hiyo nilisimama kwa mbwembwe nikisema maneno ya Mtakatifu Paulo, "Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza..." (2 Timotheo 4:7) Basi akasomwa hadi mtu wa mwisho. Kila nikigeuka nyuma naona mstari mrefu wa wanafunzi wenzangu ukinifuata huku mbele yangu akiwepo mwanafunzi mmoja tu. Somo la kilatini nilipata alama 79. From zero to 79 ain't a simple work my dear.
Toka siku hiyo nikasema, "Kufeli mtihani na kufaulu ni maamuzi." Sijawahi kufanya makosa tena.
Leo hii zero ndiyo inaniwafanya nitembee mashuleni na vyuo mbalimbali nikisema, "IT IS POSSIBLE, TO ME FAILURE WAS NEVER FINAL."
Funzo:
Magumu unayopitia Leo, inawezekana ndiko Fursa uanayotakiwa uitatue ilikojificha. Usilalamike kwa kupata mizigo mizito maishani, mwombe Mungu akusaidi mabega imara ya kuibeba mizigo hiyo.
Sehemu itakayofuta nitaelezea jinsi dasara langu lilivyopata tuzo ya NECTA kidato cha NNE. Usikose....
Ndimi:
#KijanaWaMaarifa
Edius Katamugora
0764145476
0758594893
ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
0 comments:
Post a Comment