Tuesday, 14 August 2018

VIJANA TUNAKWENDA WAPI?

Mojawapo ya kitu ninachojivunia ni kupata Fursa ya kujuana na watu wapya na kuongeza mzunguko wa marafiki.

Wiki iliyopita kuna kaka mmoja alinifuata inbox WhatsApp akaniambia "Kaka unaandika mambo ambayo Vijana wengi tunayaona ya kawaida lakini kiukweli wengi wamepotea. Huku nilipo field kuna Vijana wengi wanawaza kuajiriwa, yaani akihitimu chuo apate ajira chap." Mimi nikamwambia kuna haja ya kusema kwa nguvu kubwa "Mambo yamebadilika." Kama hujui kwamba mambo yamebadilika basi jua kupitia makala hii.

Ukifika vyuoni unakutana na watu wengi wenye ndoto za kuajiriwa Mara tu wakimaliza chuo kumbe mambo hayako hivyo. Hivi unajua kwamba kila mwaka wanahitimu watu zaidi ya milioni moja na wanaopata ajira kila mwaka hawazidi laki 3. Unajua kwamba zaidi ya 80% ya Vijana wanajihusisha na kilimo.

Hizo ni taarifa tu nakupa ili ushtuke. Inauma sana unakutana na mtu anasema, "Yaani nahisi kuumwa nikikosa bando ya kusoma umbea wa Insta." Serious? Una ndoto wewe? Kweli mtu wa hivi ana malengo. Vijana wengi wanajua kufuatilia maisha ya watu wengine zaidi ya wanavyofuatilia maisha yako.

Hebu kaa chini na tizama kwenye simu yako una watu wangapi ambao wanaweza kutatua matatizo yako. Kwenye kurasa zako za mitandoa ya kijamii una watu wangapi ambao mnafahamiana wenye majibu ya maswali unayojiuliza kila siku.

Usikae kae tu ili mradi siku zinaenda. Teknolojia inawaacha watu wengi. Kaa chini na jiulize ni kwa kiasi gani utaweza kukuza ujuzi wako.

Kila siku chukua muda wako wa ziada jiulize maswali haya:
1. Nitawezaje kufanya zaidi ya Jana?

2. Nitawezaje kuwa na matumizi sahihi ya muda.

3. Nitawezaje kuongeza thamani mahali nilipo?

4. Nitawezaje kuongeza uzalishaji katika mambo ninayoyafanya?

Ndimi:
Edius Katamugora
#KijanaWaMaarifa
0764145476
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: