Mtoto
anapoanza kutembea huanguka mara nyingi lakini hicho hakiwi kikwazo cha yeye
kuacha kujifunza kutembea.
Katika
maisha yetu ya kila siku tunapoanza kufanya kitu huwa tunakutana na changamoto
mbalimbali. Iwe katika biashara, ujasiriamali, katika elimu na katika kutumia
vipaji vyetu tunapata ugumu tunapoanza. Ndiyo maana nikaandika Makala hii yenye
kichwa cha MWANZO MGUMU.
Ugumu
unaoupata mwanzo katika safari yako iwe ya kutumia kipaji chako au ujasiriamali
au katika elimu unakukomaza na unapata kuwa mtu imara. Kuna msanii Kelly Clarkson kwenye wimbo wake wa ‘Stronger”
aliwahi kuimba akisema, “Kisichokuua
kinakukomaza.”
Ili
roketi iruke kutoka ardhini kwenda angani katika dakika tatu za mwanzo utumia
mafuta mengi sana kuliko mafuta yanayotumika katika safari yake yote. Wakati
unaanza unahitaji kutumia nguvu nyingi kama roketi lakini ipo siku nguvu hizo
utafurahia ugumu wa mwanzo. Hakuna hadithi nzuri ya ushindi kama iliyopitia
katika magumu na kuyashinda.
Unapoanza
kutumia kipaji chako watu watakubeza, watakutukana, watakusengenya, watakusema
lakini hayo yasikuvunje moyo, katika biashara na ujasiriamali hivyo hivyo.
Unahitaji kukomaa na kuwa imara. Ipo siku utafurahia na mambo yatakuwa rahisi
kama utakuwa mtu asiyekata tamaa.
Ulipokuwa
darasa la kwanza moja kutoa tano ulisema haiwezekani
hivyo ilikuwa na hesabu ngumu kwako, lakini ulipofika darasa la tano, moja
kutoa tano ilikuwa hasi tano. Ugumu uliionekana mwanzo ulipata jibu. Katika
maisha yetu mwanzo uonekana mgumu lakini kadri unavyoendelea kujifunza na
kufanya kazi kwa bidii mambo magumu huonekana mepesi.
Inawezekana
leo unaona mambo yako ni magumu na hayendi, jipe muda na usikate tamaa. Kuna
watu wengi walikata tamaa juu ya ndoto zao kumbe walibakiza hatua kidogo
kufikia ndoto hizo. Fikiria Thomas Edson alifanya mazoezi ya kutengeneza balbu
ya umeme mara zaidi ya 1000 na jaribio la 1001 ndiyo lilifanikisha leo hii
dunia inatumia taa za balbu, hii imepelekea watu kuweza kufanya kazi masaa 24
kwani hapo kabla ya taa za umeme kuwepo mambo ya kufanya kazi saa 24 hayakuwepo. Mwanzo mgumu ni ishara ya kwamba
njia uliyopo ni sahihi.
“Mafanikio
yako mikononi mwako.”
Ndimi
#KijanaWaMaarifa
Edius
Katamugora
0764145476
0758594893
ekatamugora@gmail.com
0 comments:
Post a Comment