Umewahi kuona watu wakitoa shuhuda makanisani katika ibada mbalimbali zinazooneshwa kwenye televisheni. Yaani mtu alikuwa anaumwa ugonjwa Fulani, akaombewa baada ya muda anarudi kutoa shuhuda kwamba amepona.
Kitu ambacho hutokea hapo ni kwamba watu wengi huamini. Na utakuta idadi ya watu wanaotaka kuombewa huongezeka. Watumishi msinielewe vibaya kuna kitu nataka kufundisha hapa.
Hebu sasa turudi kwenye biashara. Kama unafanya biashara bila shuhuda, basi bado haujajua kuuza. Bado haujawa gwiji katika mambo ya mauzo. Nimekuwa nikiona wafanyabiashara wengi na wajasiriamali wengine wadogo na wengine wakubwa wakitangaza bidhaa zao bila kutumia shuhuda. Testimonies.
Ninaposema shuhuda namaanisha nini?
Ukitaka kutumia shuhuda kujitangaza, tumia picha za watu wakitumia bidhaa zao. Usiweke bidhaa zako tu katika matangazo au mitandao ya kijamii bila kuonesha picha za watumiaji. Waombe wateja wako wapige picha wakiwa na bidhaa yako. Aisee ni bonge moja la tangazo. Linazinidi hata matangazo ya graphics.
Ngoja nikwambie kitu, dunia ya Leo ambayo watu wengi wanapenda kuonekana, ukimposti mtu anatumia bidhaa yako, watu wengine watahitaji kupostiwa Ili nao waonekane. Ukiwaposti wanatumia bidhaa zako wewe tayari umeshauza.
Makampuni makubwa yamekuwa yakitumia watu maarufu waonekane wanatumia bidhaa na huduma zao ili wawavutie watu wengine. Hizo ni testimonies/shuhuda. Leo hii unaona Nandy anawatangaza halotel the issue behind ni kujaribu kuwavuta watu watumie halotel kwasababu Nandy ni msanii maarufu na ni msanii anayependwa na watu. Unaweza pia kuwatumia watu maarufu katika matangazo yako au wakiwa katika pozi la picha wakitumia bidhaa au huduma yako. "Kama unataka kuiona biashara yako mbali Fanya biashara kama kwamba unashindana na makampuni makubwa kama IBM, Google, Apple na Nike." Anasema Mark Cuban mwandishi wa kitabu cha How To Win At The Sports Of Business.
Kama una ndoto ya kufika mahali pakubwa Fanya biashara kama kampuni kubwa. Tumia testimonies kila unapotangaza biashara yako.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
#KijanaWaMaarifa
0764145476
0758594893
ekatamugora@gmail.com
0 comments:
Post a Comment