Kati ya vitu ambavyo utakuta natumia nguvu nyingi kuvitafutia maarifa na kuvielewa kwa mapana zaidi ni matumizi ya mitandao ya kijamii.
Nimekuwa nikifanya hivyo kwasababu mitandao ya kijamii imekuwa si kitu cha kukubali kikupite hivi hivi kwani kimebeba uchumi mkubwa katika karne hii ya taarifa.
Kuna watu wanatengeneza pesa kubwa kupitia mitandao ya kijamii. Lakini vilevile kuna wengine wanakopa waweke vocha katika simu zao ili watizame umbea au wafuatilie skendos za watu mbalimbali maarufu. Kuna msanii aliwahi kuimba, " you don't make money, you don't make sense." hautengenezi pesa kupitia mitandao ya kijamii, you don't make sense. Inashangaza kuona mtu ana followers elfu 6 Instagram halafu unakuta anakwambia eti ana biashara haina wateja. Serious?
Unawafollow wakina nani? Unawafuatilia wakina nani?
Binafsi nimejijengea tabia ambayo inanifanya nifunguke na nijifunze vitu vipya kila kukicha. Nikiona MTU ni mwandishi na anafanya kazi kama zangu lazima nimfollow au nimuombe urafiki? Je wewe watu wa Industry yako umejenga urafiki nao. Kuna watu wangapi ni wafanyabiashara kama yako umewafollow Instagram, au unawafuatilia wanamuziki? Kama hakuna tafadhari achana na makala hii nenda kawafollow Mara moja, nenda kawaombe urafiki Mara moja.
Waingereza wanamsemo mzuri usemao, "Mind your own business. " kwa lugha rahisi naweza kusema, "Jali biashara yako." Anza kufuatilia watu wanaofanya kitu kama unachokifanya. Huko utaweza kujifunza mambo mengi kwenye industry yako na unaweza kupata hata mawazo ya kuiba(ndio kuiba, usishangae kwanini nasema hivyo. Hivi unajua kwamba staili ya Michael Jackson ya kucheza kwa kurudi nyuma aliiiba kwa watoto wa mtaani) . Kama ni mwanamuziki fuatilia wanamuziki wenzako, sio tunakuta wafuasi wako wakubwa ni wacheza Mpira. Hakuna chochote unachofaidi huko. Mind your own business my dear.
Usitumie nguvu nyingi kufuatilia watu ambao hata sikumoja hautakuja kukaa nao stage moja(NB: sisemi kwamba usiwafollow watu)
Siku moja Mchezaji maarufu wa kikapu kutoka Marekani Kobe Bryant aliulizwa siri yake ya mafanikio ilikuwa ipi, yeye akasema, "Toka nikiwa mdogo nilikuwa nikitumia muda wangu mwingi kutizama wachezaji wengine mashuhuri walivyokuwa wakicheza hatimaye nimekuwa hivi nilivyo Leo."
Unachukua muda gani kuwatizama watu wanaofanya kitu unachotarajia au unachokifanya?
Ndimi:
Edius Katamugora
#KijanaWaMaarifa
Instagram: ediuskatamugora
0764145476
0758594893
ekatamugora@gmail.com
0 comments:
Post a Comment