Tarehe 24 mwezi wa kumi na moja mwaka huu ilikuwa siku ya
furaha sana kwangu. Ni siku niliyotoa kitabu change cha pili baada ya kile cha
kwanza kinachoitwa BARABARA YA MAFANIKIO.
Kitabu hicho kinaitwa NAMNA YA KUWA MTAALAMU UKIWA BADO
UNASOMA.
Mtaalamu ni nani?
Mtaalamu ni mtu mwenye elimu, ustadi au ujuzi wa fani au
jambo Fulani maalumu. Tunaweza kuwa na mhadisi mtaalamu, mama ntilie mtaalamu,
muuzaji mtaalamu, mchezaji mtaalamu, mwanasheria mtaalamu, mwalimu mtaalamu,
kutaja wachache.
Kimsingi wataalamu ni watu wanaofanya mambo kwa ubora na
upekee. Kuwa mtaalamu ni moja kati ya kitu kikubwa ambacho unatakiwa kuwa nacho
katika karne hii. kama una kiu ya kuwa mtaalamu kitabu cha NAMNA YA KUWA
MTAALAMU UKIWA BADO UNASOMA (HOW TO BECOME AN EXPERT WHILE AT SCHOOL) ni jibu
tosha la kiu yako.
Kuna watu wengi wanatamani kuwa wataalamu katika sekta
mbalimbali lakini hawajui waanzie wapi. Kitabu hiki kinakupa dira ya wapi
uanzie ili uwe mtaalamu au gwiji katika sekta ya ndoto yako.
Katika karne hii
ya ishirini na moja tuliyomo, wataalamu ni watu wanaohitajika sana, kila mtu
anahitaji kazi yake ifanywe na mtaalamu, kila mtu anatamani ahudumiwe na
mtaalamu, kila mtu anatamani kuambatana na mtaalamu, kila kampuni
inatamani kuwa na wafanyakazi wataalamu.
Lengo la
kuandika kitabu hiki ni kuwasaidia watu wote wenye ndoto za kuwa wataalamu
katika fani mbalimbali au jambo fulani maalumu waweze kutimiza ndoto zao.
Fikiria unaingia katika chumba fulani chenye watu wengi na wanakutambua kwa
utaalamu ulio nao. Ni jambo jema na la kujivunia.
“Hauwezi kuwa mtaalamu ndani ya
siku tano,” ni methali ya kiafrika. Kuwa mtaalamu kunahitaji muda wako, nguvu
zako, akili zako na kujitoa kwako. Kila mtu unayemuona ni mtaalamu katika eneo
fulani kuna siku alikuwa ni mtu mpya kwenye hali hiyo ambayo leo hii inamfanya
aonekane mtaalamu.
Utaalamu ni kitu
unachoweza kujifunza kama ulivyojifunza kusoma na kuandika au kutembea na
kuongea. Kuanza kujifunza utaalamu mapema ni jambo la busara mno katika chaguzi
zako unazoweza kuzifanya katika karne hii, hasa ukianza kujifunza namna ya kuwa
mtaalamu ukiwa unasoma ili ukija kuhitimu tayari unaweza kusimama kama mtaalamu
kinara. Watu wakihitaji mtaalamu wewe uwe wa kwanza. Dunia ya leo inawapokea
wataalamu kwa mikono miwili hivyo ni jukumu lako leo kuanza kujifunza namna ya
kuwa mtalaamu.
Kitabu hiki
nimekigawa katika sehemu huu tatu; Sehemu ya kwanza inaeleza mbinu mbalimbali
zitakazokusaidia kufaulu mitihani. Mbinu hizi nimezitumia mimi na zimenipa
matokeo makubwa lakini pia katika sehemu hii nimehadithia nilivyowahi kupata
sifuri darasani na hatimaye kutoka sifuri hadi kupata maksi za juu na kuwa mtu
wa pili darasani. Hii ni historia ya kusisimua niliyoiandika ili kumhamasisha
mwanafunzi yeyote aliyekata tamaa kuwa anaweza kufanya vyema darasani kama mimi
niliweza yeye pia anaweza.
Sehemu ya pili
ya kitabu hiki ndiyo iliyobeba kichwa cha kitabu hiki; Namna Ya Kuwa Mtaalamu
Ukiwa Bado Unasoma. Hapa nimeeleza mbinu mbalimbali anazoweza kuzitumia mtu
yeyote kuufikia utaalamu. Katika sehemu hii nimetumia misemo mingi ya
kukuhamasisha na mifano hai ya watu ambao leo ni wataalamu katika sehemu
mbalimbali.
Sehemu ya tatu
ya kitabu hiki nimeiita Shule Y a Pesa. “Kama
shule zingepewa jukumu la kuwafundisha watu kuongea na kutembea, wengi
wangekuwa mabubu na viwete,” alisema Herbert Kohl, mwandishi wa vitabu.
Hakuna shule yeyote hapa duniani ambayo hutoa elimu ya pesa hivyo nimeona
kitabu hiki kiwe sehemu muhimu ya kutoa shule hiyo maana watu wengi wameikosa
na wamekuwa wakilalamika kwanini wanakosa pesa au hawana pesa. Kama wewe ni
mmojawapo wa watu hao, sehemu hii ni mkombozi kwako. Kama ulikuwa ni mgonjwa
mahututi, sasa umepata dawa. Usisite kuimeza.
Katika sehemu hii ya tatu, nimeongelea
pia biashara na ujasiriamali. Watu wengi wanapenda kuwa wafanyabiashara na
wajasiriamali lakini hawajui waanzie wapi. Kitabu hiki kimekufunulia baadhi ya
mambo yatakayokufungulia njia katika biashara na ujasiriamali.
Baadhi ya watu waliosoma kitabu hicho wamesema yafuatayo;
“Kaka kusema kweli hiki kitabu nahisi kubarikiwa aisee
nashukuru sana andaa kopi moja kwa kaka yangu wa Songea au kama yuko Songea
nambie namna atakavyokipata kiko vizuri Zaidi ya nilivyotegemea shukrani
sanaaaa.” Ota Oscar- Mbeya
“Interesting Book. Page 162 now. This is an important broke
of house mind.” Saada Mpandachalo
“Kitabu kizuri sana.” Ronah Ernest
“Habari Mr Edius Katamugora, baada ya kumaliza kusoma kitabu
chako cha “Namna ya kuwa mtaalamu ukiwa bado unasoma” nimejifunza mengi mno. Hiki
ni kitabu ambacho natamani kila kijana aliyeko chuo kikuu anastahili kukisoma,
hasa kwa wakati hu ambapo ajira ni fumbo la maisha, ajue ni nini cha kufanya. Bei
ya kitabu hiki na yaliyomo haviwiani kabisa, thamani yake Yazidi elfu kumi na
tano. Kaka Edius nakuona mbali zaidi ya hapa.” S. A Marandu.
Kitabu hiki kinapatikana kwa bei ya shilingi 15000/= tu unaweza
kuwasiliana na mawakala wetu walioko karibu nawe ili upate kitabu chako mapema
iwezekanavyo:
Dar es Salaam:
Chuo cha ARDHI: O757 082 633
Kariakoo: 0757 443 217
Morogoro (SUA)
0755 848 633
Arusha:
0764 771 298
Dodoma;
0685 097 713
Moshi;
0685 097 713
Mbeya:
0764 145 476
Mwanza:
0744 581 476
Karibu sana ujipatie kopi yako sasa.
Edius Katamugora
0764 145476
Ekatamugora@gmail.com
0 comments:
Post a Comment