Unahitaji kujiamini ili uwe mwanaharakati bora, unahitaji kujiamini kabla ya kuanzisha biashara yako. Unahitaji kujiamini ili ufanye chochote kifanikiwe.
Fikiria mtu kama Baraka Obama ambaye alikuwa rais wa kwanza Mmarekani mweusi. Huyu alikuwa akishindanishwa na kina Hillary Clinton ambaye alikuwa tayari First Lady wa Marekani. Hakukuwa na histori yoyote ya mtu mweusi kuwania urais wa Marekani. Obama alijiamini ipasavyo na kushinda.
Kuna mtu aliwahi kusema, "Kujiamini, kujiamini, huo ni mtaji." Na mwingine akaongeza akisema "Kujiamini na utaalamu, ni jeshi lishiloshindwa."
Unahitaji kujiamini ili ufanikiwe.
Hauwezi kuwa kiongozi bora kama haujiamini. Hauwezi kusimamisha biashara kubwa kama haujiamini, hauwezi kuwa mbunifu bila kujiamini.
Nikitafakari Thomas Edson aliyetengeneza taa ya umeme(balbu) kwa kushindwa zaidi ya mara 1000 ninaona kujiamini ndani yake maana bila hivyo angeshinshindwa kuendelea na kukata tamaa.
Mwaka 1860 kulikuwa na vita nchini Marekani, vita hiyo ilikuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyohusisha watu wa kusini na kaskazini.
Jeshi la kusini lilikuwa na wanajeshi mashuhuri kwelikweli liliongozwa na Robert E. Lee ambaye hakuonekana kama
Jenerali alionekana kama mtu wa kawaida. Hapa ndipo tunapoweza kusema "Bora kundi la kondoo elfu moja kuongozwa na simba mmoja kuliko simba elfu moja kuongozwa na kondoo mmoja."
Jeshi la kaskazini liliongozwa na Ulysses Grant, jeshi hilo lilikuwa na wanajeshi wachache. Grant alionekana kama generali haswa.
Unajua nini kilitokea, jeshi la Grant lenye wanajeshi wachache lilishinda. Grant alijiamini ndiyo maana alishinda vita ile.
C ya kwanza ni courage= ujasiri.
Ujasiri ni mojawapo ya mahitaji yanayomfanya mtu ajiamini.Fikiria uanatamani kuongea mbele za watu. Lazima uwe jasiri kufanya mambo hayo.
Au wewe ni mnene sana unatamani kuanza kufanya mazoezi. Unahitaji ujasiri wa kuogopwa kuchekwa na watu na kuanza kwenda jimu na kadhalika.
C ya pili ni "Commitment"
Kuwa Commited kwa kiswahili naweza kusema ni "Kudhamiria." Ili ufanye kitu chochote lazima uwe na nia, lazima udhamiria.
Nia yako ndiyo itakufanya ufanye mambo makubwa ambayo wengine wanaweza kuona kama hayawezekani. Kwamfano wanariadha hudhamiria kabla ya kuanza kukimbia kuwa watashinda, kule kudhamiria kunakufanya ujiamini na kukimbia kwenye spidi zaidi ya mwanga wa radi kama anavyopenda kusema Usain Bolt
C ya tatu ni "capabilities." Uwezo.
Ili ufanye kitu fulani uwe na uwezo wa kukifanya.
Ili ufanye kitu fulani uwe na uwezo wa kukifanya.
Mfano kama unahitaji kuwa mwandishi lazima uwe na uwezo wa kuandika, utatafuta mtu aliyefanikiwa kwenye uandishi.
Bila kudhamiria hauwezi kuwa mtu wa kujiamini.
Bila kudhamiria hauwezi kuwa mtu wa kujiamini.
C ya nne ndiyo sasa "Confidence" hufuata.
Unahitaji hivyo vitu vitatu vya mwanzo yaani, courage, commitment na capabilities ili kujiamini.
Unahitaji hivyo vitu vitatu vya mwanzo yaani, courage, commitment na capabilities ili kujiamini.
COME & SEE
Edius Katamugora
#KijanaWaMaarifa
0764145476
ekatamugora@gmail.com
#KijanaWaMaarifa
0764145476
ekatamugora@gmail.com
Unaweza kupata vitabu vyangu kupitia namba 0764145476
0 comments:
Post a Comment