Nilitamani kuandika makala hii nyuma kidogo lakini sikupata muda lakini nafikiri leo ndiyo siku Mungu alipanga iruke hewani, kwa maana binadamu tunapanga na Mungu anapanga.
Tuyaache hayo, twende kazi...
Siku nyuma kidogo nimekuwa nikiwauliza watu maswali haya:
1. Unatumia facebook?
2. Au ntauliza facebook unatumia jina gani?
2. Au ntauliza facebook unatumia jina gani?
Majibu ambayo huwa nayapata huwa yananiacha mdomo wazi.
Utasikia mtu anasema, "Facebook ni ya watoto." au "facebook
hainogi." Aliyenifurahisha zaidi alisema, "Niliacha kutumia facebook
baada ya kugundua hata ma house girls wamejaa huko."
"It's ok, it's ok" (In Pierre's voice)
Unasema Facebook ni ya watoto lakini bado haujaona umuhimu
wake. Binafsi nimekuwa nikifuatilia mambo mengi kuhusu mitandao ya
kijamii. Natumia muda mwingi kuielewa na kuisoma kwa makini.
Jibu ninalokupa leo ni kwamba facebook sio ya watoto. (Naomba uwatag wote waliowahi kukuambia majibu kama hayo hapa.)
Kama facebook ni ya watoto kina Strive Masiyiwa wasingejisumbua kuja huku kuandika mambo mengi kuhusu biashara.
Huyu mzee ukimfuatilia huwa hajibu comments Instagram
lakini huku Facebook anajibu kila comment anayoona inafaa. Bado unasema
huku kumejaa watoto?
Biashara nyingi unazoona zimekua ni kutokana na wateja
kutoka huku facebook. Binafsi nimetengeneza fan base kubwa facebook
kuliko kwingine.
Endeleeni kusema facebook ni ya watoto.
Je unayajua haya?
Leo hii kama facebook ingekuwa nchi, ingekuwa nchi ya
kwanza duniani kwa kuwa na idadi ya watu wengi. Facebook inawatumiaji
bilioni 2.38 kwa mwezi, wakati nchi ya China yenye watu wengi
inakadiriwa kuwa na watu bilioni 1.4
Watu milioni 1.56 huingia katika account zao kila siku. Huku ongezeko likiwa asilimia 8 kila mwaka.
Watu wengi wanaotumia mtandao huu ni kuanzia miaka 25-34, ambao ni asilimia 29.7 ya watumiaji.
Kila sekunde profiles tano mpya hufunguliwa.
76% ya watumiaji ni jinsia ya kike ya 100% ya wanawake na 66% ya watumiaji ni wa kiume wakitoka katika asilimia 100 ya wanaume.
Watu wengi huwa online kuanzia saa saba mchana hadi saa
tisa alasiri. Ukipost sa 7 watu wengi wataona kuliki ukipost saa
8.(chanzo Forbes)
Siku za Alhamisi na Ijumaa watumiaji huwa ni wengi mno, ongezeko likiwa asilimia 18.
Kila siku picha milioni 300 huwekwa kwenye mtandao wa Facebook.
Wastani wa kila mtu kutumia facebook ni dakika 20.
Kila sekunde 60 kwenye facebook comments 510000 huandikwa
na status 293000 huwa zinakuwa updated na picha 136000 huwekwa facebook
(Chanzo: The social Skinny)
Asilimia 50% ya vijana wenye umri kuanzia miaka 18-24 huwa wanaingia Facebook mara tu waamkapo. (Chanzo: The social Skinny)
42% ya wafanyabiashara wanasema facebook ni ya muhimu sana katika biashara zao.
Bado unaichukulia poa facebook?
Kupitia facebook nimepata marafiki wengu, wateja wengi na
nimejifunza vingi. Facebook ni darasa tosha la maisha, (Kwa watu serious
lakini).
Kupitia facebook unaweza kutangaza biashara yako kwa bei
rahisi, hata kwa kupitia ukurasa wako na bado ukapata wateja. Waliokuwa
mnasema facebook ni ya watoto, mnakwama wapi?
Sehemu nyingine ambayo nakushauri ujiunge ni Twitter, kama
hauna account kuwa nayo sasa utajifunza mengi. Unaweza kunifollow pia
kupitia @katamugora
Rudi facebook kumenoga.
Ndimi
0 comments:
Post a Comment