Kama kuna tabia ambayo tunapaswa kuanza kuijenga ni kuamka na kufanya mambo yako kabla ya kushika simu.
Simu hizi ni nzuri lakini tabia ya kuamka na kutizama mtandaoni kuna nini imekuwa ikitugharimu sana.
Kwa mfano ukiamka na mood ya kutosha ukashika simu yako na
kukuta habari mbaya tayari siku yako itakuwa imeharibika kwa kiasi
fulani.
Au ukiamka na nguvu ukashika simu yako na kukuta ujumbe wakukuhuzunisha nguvu zako mara moja zitakwisha. Hata kama una mipango mingi kwa ajili ya siku husika lazima mipango yako ivurugike.
Hakikisha walau dakika 30 za kwanza baada ya kuamka haushiki simu na unajiweka bize na mambo ya msingi.
Ukiifanya hiyo iwe tabia yako itakufanya ufanye mambo mengi kwa weledi mkubwa na uzalishaji utakuwa mkubwa.
Asubuhi kabla ya kushika simu yako kuna mambo mengi ya
kufanya; kusali, kufanya mazoezi ya viungo, kujisomea kitabu, kufanyia mazoezi
kipaji chako, kupata kifungua kinywa, na kutafakari. Kutaja machache.
Ifanye asubuhi yako kuwa njema kwa kuepuka habari mbaya. Kumbuka, "Maisha huanza asubuhi," kama anavyosema Pastor Joel Osteen.
Kama maisha huanza asubuhi kwanini huanze kwa kupoteza thamani ya maisha kila kunapokucha?
Njia nyepesi ya kuamka na kutoshika simu ni kuweka simu
yako katika flight mode muda unapokwenda kulala, hata kama unasoma kitabu chako kupitia nakala
tete hautakuwa na muda wa kusumbuliwa na mtu kupitia ujumbe mfupi (sms)
, au kupigiwa simu au ujumbe wa whatsapp na mitandao mingineyo.
, au kupigiwa simu au ujumbe wa whatsapp na mitandao mingineyo.
Mara nyingi pia mitandao ya kijamii imekuwa ikila muda wetu mwingi wa asubuhi. Hilo sio jambo jema.
Ukiwa mtumiaji mkubwa wa mitandao ya kijamii kwa muda
mwingi unakuwa kama mlevi wa pombe au mvutaji sigara. Kuna kemikali
inayoitwa Dopamine ambayo huzalishwa na ubongo.
Kemikali hiyo hukufanya
mtu ujisikie vibaya kama haujaingia mtandaoni. Unakuwa mlevi wa
mitandao. Mitandao ya kijamii haikujengwa ili sisi tuwe walevi wake.
Ugonjwa ambao watu wengi wanao unaitwa FOMO(Fear Of Missing Out) kwa kiswahili tunaweza kusema ugonjwa wa kutaka kila kitu kisipite bila wewe kujijua, kama asemavyo Austin Kleon mwandishi wa vitabu. Huo ni ugonjwa unaowatafuna watu wengi.
Dawa ya ugonjwa huo inaitwa JOMO (Joy Of Missing Out) yaani furaha ya kukosa baadhi ya vitu. Sio kila kitu kinachowekwa mtandaoni lazima ukione au ukisome. Niliwahi kusema siku za nyuma, "Mitandaoni kuna mambo mengi, chambua ni yapi uchukue (yanayokuhusu na ya muhimu) na mengine yaache kama yalivyo"
Mitandao haikujengwa ili itutumie, iliwekwa ili tuitumie lakini maajabu ni kwamba sasa inatutumia. Inasikitisha sana.
Jaribu kupunguza matumizi mengi ya mitandao ya kijamii.
Ifanye asubuhi yako kuwa njema kwa kutoamkia mtandaoni. Fanya mambo ya
msingi kwanza unapoamka. Yaliyopo mtandaoni yatabaki kuwapo na hakuna
litakalo kupita.
Ndimi
Edius Katamugora
#kijanawamaarifa
0764145476
ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
#kijanawamaarifa
0764145476
ekatamugora@gmail.com
0 comments:
Post a Comment