Headlines
Loading...

Thursday, 25 July 2019

INTERNET IS THE FUTURE



Jumanne ya tarehe 22 Julai mwaka 2019 nilipata fursa ya kufundisha somo linaloitwa INTERNET IS THE FUTURE katika kundi la whatsapp lijulikanalo kama CYM International

Yafuatayo ni baadhi ya yale niliyoyafundisha.

Nimechagua somo la intaneti kwa sababu kuu moja. Imebeba maisha yetu makubwa lakini bado hatujashutka. Bado tumelala. Kama kuna walioamka katika matumizi ya intaneti ni wachache. 

Pointi ya kwanza kabisa ya kuanza nayo darasani.

*Kama haupo kwenye intaneti, hauishi, kama biashara yako haipo kwenye intaneti haiishi. Imekufa.*

Njia nzuri ya kuwa kwenye sehemu nzuri ya kuununua wakati ujao(buying the future) ni kuwa kwenye intaneti.Nimekua nikiwaambia watu, na nimeandika sana. Badala ya kuitumia intaneti yenyewe inatutumia. 

Nilisoma Twitter wakati fulani zaidi ya asilimia 80 ya watu hutumia intaneti vibaya huku asilimia 20 tu ndio hufaidika tu.
 
Intaneti haikuwekwa itutumie bali tuitumie, habari mbaya ni kwamba watu wengi inawatumia.

Kuna faida nyingi za kutumia intaneti:
 
Mfano, kupakua vitabu vya kusoma, kama unapenda kujifunza kwa video unaweza ingia youtube. Kikubwa zaidi kuna online Courses nyingi zinatolewa but watu wengi hatujui, Kama nilivyotangulia kusema leo kama biashara yako unayoifanya haipo mtandaoni biashara hiyo haipo. It doesn't exist.

Tumeshuhudia makampuni mengi makubwa ambayo yamekuja miaka ya hivi karibuni, lakini yamekuwa makampuni tajiri sana duniani na yamegusa maisha ya watu.

Kuanzia
AMAZON
FACEBOOK
ALIBABA
KIKUU
YOUTUBE
UBER
TAXIFY.
NETFLIX
 
Leo hii watu wengi wanatumia intaneti. Baishara nyingi zipo mtandaoni. Watu wengi wanashinda kwenye intaneti. Huko ndipo macho ya watu yalikohamia.

Kuna msemo usemao, "Biashara huenda kule macho yanapokwenda."

Kama macho yapo kwenye mtandao hatuna budi sisi wafanya biashara tuwe kwenye mitandao pia.

Kama watu wanajua unachokifanya kwenye mitandao watakua tayari kuwaambia wengine kuhusu wewe. Nzuri  zaidi unaweza fikia watu wengi zaidi. Nafikiri umewahi ona kwenye matangazo wanasema "Na mikoani tunatuma."

Kwenye mitandao ya kijamii kama unafanya biashara kwanza lazima ujue wateja wako wanapendelea nini. Sio wewe unapendelea nini (mtandao). Kwa mfano kama ni mwandishi ni rahisi sana kupata wateja wa kazi zako kama unatumia:
 
Facebook Twitter na Linkedin. Anayeuza bidhaa ni rahisi sana Instagram kuliko Twitter.

Njia ya kwanza ya muhimu ni kujua wateja wako wanapenda nini. 

Hapa whatsapp ni rahisi kuwa na darasa kuliko insta au kwingineko. Mfano:
 
Kama ni mwandishi ni rahisi sana kuwapata wasomaji Facebook na whatsapp kuliko Instagram ambapo watu wengi huangalia picha. 

Watumiaji wengi wa insta huwa hawasomi captions.

Sasa unawatekaje watu wakujue.?

Kwenye mitandaoni kila kitu ni Kujulikana watu wengi wakikujua umetusua. Kama hawakujui hakuna jipya utakalopata.

Kitu kimoja muhimu kwenye social medias:

*Content Content Content content*

Kwa kiswahili tunasema Maudhui.

Maudhui yako lazima yawe yameshiba. Kama unauza viatu, je wewe ni mkali wa fashion?

Kama unachora, je una michora ya kuwavutia watu?

Watu wengi hawatengenezi *content bora* wanakimbilia kuuza.

Nitoe mfano tu. Mange Kimambi ni content creator wa kujua watu kiundani hivyo hivyo watu wa shilawadu.

Millard ni content creator wa habari na matukio.

Joti ni content creator wa vichekesho.

Wewe ni content creator wa nini??

Kuna watu wanajiuliza, labda mimi nauza Asali. Natengenezaje maudhui?

The best way ni kuwafundisha watu.

Mimi naandika makala zangu bure kwenye mitandao hapo kuna watu nawafanya wanakuwa wafuatiliaji wangu wa kila siku. Hawa baadaye huwa wateja wa kazi zangu.

Unawafundishaje?

Kwa mfano muuzaji wa asali.

Wafundishe watu umuhimu wa kutumia asali. Ni mambo gani watakosa kama hawatumii asali, n.k

Toa elimu ya bure kuhusu bidhaa yako.

*Kosa la watu wengi wanatoa matangazo ya bidhaa tu bila kutoa maelezo kama hayo*

Au unauza nguo, suruali za kadeti.

Watolee watu sababu za kuvaa kadeti za Geep, au Zara badala ya kuvaa Polo. Ni mfano tu. Lakini inakuonesha ni kiasi gani kwenye mambo ya fashion umeiva.

Watu huwa wanawafuatilia wale walioiva/waliobobea katika masuala wanayoyafanya.

*People will follow you in your area of competence.*

Watu wanaohusika na mambo ya branding kwenye mitandao. Unaweza kupata watu wa kuaminika wanaokufuatilia kwa kipindi cha miezi 6 mfululizo. Haiji kwa usiku mmoja.

Kila kitu kina gharama. "Hauwezi kuwapa mimba wanawake 9 ukategemea wajifungue ndani ya mwezi mmoja." (Warren Buffet)

Leo hii kila mtu anapost kwenye mitandao ya kijamii. Kila sekunde, kila dakika, kuna content mpya hutengenezwa.

Lazima utengeneze njia ya kuonekana. Kama huonekani hauwezi kupata fan base ya uhakika.

So you need tu post at least ten pieces of contents daily Kama haufanyi hivyo wenzako na wanafanya na wanateka watu. Ipo wazi kuwa kila mtu anataka kuonekana lakini wanaonekana wale wanaokimbia na muda na wanaopost sana. Nikupe Assignment ndogo, hebu kaangalie Millard Ayo kwa siku anapost mara ngapi.

Wakati unapost hivi vitu kumi hakikisha vina uzito. Usifanye kwasababu Edius kasema eti nionekane. Watu wanafuata vitu bora na si bora vitu.

Wanaofanya kwa ubora ndiyo wanaoshinda.
Be different
Be exceptional. Usifanye kama mtu fulani anavyofanya. Tafuta vyako na stick kwa vyako, wanaopenda vitu kama hivyo watakuja. Dunia hii ina watu wengi kila mmoja anaweza fikia watu wake na maisha yakaenda.

"The internet is a copy machine" (Kevin Kelly)

Chochote unachoweka kwenye mitandao kinaweza kuwa kopidi na kusambazwa mara nyingi. So be careful with what you post. Je unapost vitu ambavyo mzazi wako au bosi wako akiviona hata ona haya ya kukufahamu.

Before you post anything ask yourself this question "I am posting this so what?"

Ukiona unapata majibu yasiyoeleweka please usiposti.





Nimalizie  kwa kusema kwamba "Mambo madogo yakifanyika kwa muda mrefu huwa makubwa."

Anza kidogo kidogo utafika pakubwa. Hakuna njia nyingine ya kuanza nia kuanza kuanzia sasa.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: