Wednesday 6 May 2020

ELIMIKA NA EDIUS (5)

Mfahamu Thomas Edison Mguduzi wa Balbu ya Umeme na Gunduzi Nyingine Zaidi ya 1000.


Umeme huwa ukikatika najua kama ulikuwa na ishu muhimu unakasirika basi unaacha taa umetegesha, ukirudi ndo unasikia, "Huoooo..."😂😂😂
Sasa behind the scene ya huoo ni jamaa anaitwa Thomas Edison.





Thomas Edison ndiye mgunduzi wa balbu ya umeme. Kabla ya kugundua balbu hiyo alifeli mara 1000 jaribio la 1001 ndio lilimfanya agundue balbu hiyo wengine wanaiita stima ya umeme.

Jambo la kushangaza ni kwamba ilimchukua takribani miaka 3 kugundua balbu hiyo. Kumbuka kwamba wanasayansi wengine walikuwa wamekwisha tumia zaidi ya miaka 50 na bado ngoma haijagundulika. Ingawaje sasa hivi unaona ni kitu simpo ila jamaa alikuwa ni mtabe.



Unaambiwa mpaka anakufa alifanya gunduzi 1093 ukiachana na 500-600 ambazo hakumaliza au aliachana nazo.




Jamaa akiwa darasa la pili mwalimu wake alimwandikia memo iliyosomeka, "Mwanao hawezi kujifunza tumemwondoa shuleni." Iliandikwa na mwalimu mkuu. Mama yake aliisoma kwa umakini barua ile na kujibu....

"Mwanangu hawezi kujifunza, nitamfundisha mwenyewe." Kusema ukweli mama wa hivi ni adimu sana hasa kwetu waafrika. Angekuwa kwenye Jamii zetu hizi mtoto wa mkulima angeambiwa, "Kaa hapa utasaidie kulima viazi shule si imekushinda."

Mfahamu William Kamkwamba Kijana Mgunduzi Toka Malawi.

Msitakae niseme kuhusu mtoto wa mfugaji, huyu angeambiwa, "Kaa hapa umekataa shule utasaidia kuchunga kondoo na mbuzi kama Daudi utatoka Goliath akipatikana."

Mida ya jioni ya saa 11:30 tarehe 10 Desemba mwaka 1914, kiwanda cha mwamba kiliungua moto na kubaki majivu. Unaambiwa majengo kumi ya kiwanda hicho yaliungua. Ukubwa wake sasa?

Chukua Old Trafford tatu ndiyo unapata ukubwa wa kiwanda hicho. Kama haujui Old Trafford namaanisha viwanja vitatu vya mpira wa miguu (acha uzito)

Edison akitazama kazi zake zikiteketea kwa moto na kuishia kuwa majivu alimwambia mwanae Charles aliyekuwa na miaka 25 maneno haya;

"Nenda kawalete mama yako na rafiki zake, hawatawahi kuona moto kama huu."

Unajua Edison kipindi hicho alikuwa na miaka mingapi? 67. Fikiria angekuwa baba yako kapigwa milioni 60 za hela ya kustaafu. Tungeenda kuzika asubuhi(just thinking). Lakini jamaa akuteteleka.

Unajua alipoteza fedha kiasi gani?

Jamaa alipoteza dola za Kimarekani $919,788 (Sawa na milioni 23 kwa dola za leo). Nimejaribu kupiga kwa hela ya kitanzania nimeshindwa kuhesabu🤣🤣🤣.

Sasa unaambiwa asubuhi yake jamaa alileta mafundi wakaanza kujenga msingi upya kwa pesa alizokopa kwa rafiki yake Henry Ford (Mwanzilishi wa kampuni ya magari aina ya Ford)




Baada ya kiwanda kuungua jamaa hakufukuza mfanyakazi hata mmoja. Alikuwa na wafanyakazi 7000.

Baada ya kujenga kiwanda upya wafanyakazi wake walifanya kazi kwa shifti mara mbili unaambiwa walizalisha zaidi ya walivyowahi kuzalisha hapo mwanzo.

Wiki 3 baada ya kiwanda kuungua Thomas Edison aligundua kamera hizi zinazowapa majina kina Hanscana na Godfather.

Funzo: Maksi zako za darasani sio maisha yako, unaweza kuwa na A darasani ukawa na F ya maisha. Pili, ukianguka simama tena, anguka mara 7 simama mara 8.

Sponsored by R'S Cakes Gallery
#ElimikaNaEdius
💎Mwisho✍🏽

Edius Katamugora
Content Creator
Creative Writer
ekatamugora@gmail.com
0764145476

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: