Ifahamu Zoom Kampuni Iliyopiga Mkwanja Mrefu Msimu Huu wa Karantini
___________________________________________________________
✒️ Kama kuna kampuni imepiga pesa ndefu kipindi hiki cha janga la virusi vya ugonjwa wa korona basi ni kampuni ya Zoom. Sio Zoom Extra iliyorekodi video ya Quarantine ya Wasafi, ninayozungumzia hapa. Amchelewi kujiongeza nyie, maana mmeambiwa akili za kuambiwa changanya na zako.
Twende kazi.
✒️ Miaka ya 80 akiwa anasoma chuo kikuu cha sayansi na Teknolojia Shandong nchini China, Eric Yuan alikuwa na mpenzi wake ambaye alisoma chuo cha mbali na alipokuwa akisoma. Mwamba akawa anasafiri kwa treni masaa zaidi ya kumi ili akamtembelee demu wake ambaye sasa ni mke wake(chezea penzi la mbali wewe).
Ikafika hatua kuna muda hawezi kumtembelea mpenzi wake (Course work zikawa zinambana) akawaza afanye nini?
✒️Ndipo akapata wazo la kutengeneza mtandao ambao watu wanaweza kuwasiliana kwa njia ya video. Chuo alikuwa akisoma hesabu na sayansi ya kompyuta.
✒️ Miaka ya 90 Bill Gates akatoa hotuba iliyotaja wakati ujao wa intaneti(Bill Gates ameandika haya pia katika kitabu chake cha Road ahead kitafute ukisome ndo utanielewa vizuri hapa) spichi hiyo ikamhamasisha sana Eric Yuan.
✒️Jamaa akasema itabidi niingie silicon Valley huko huko tukabanane mbavu na kina Elon Musk na Jeff Bezos.
✒️Akaomba visa ya kuingia Marekani wakamkatalia. Akaomba zaidi ya mara 8 ngoma bado nzito. Mara ya 9 akafanikiwa. Inawezekana jamaa msemo wa kichina usemao anguka mara 8 simama mara 9 ndio ulimsaidia.
✒️Mwaka 1997 akaingia Marekani mojakwamoja mpaka silicon valley
✒️ Oi kama ulikuwa hujui Silicon Valley ni mahali nchini Marekani ambako makampuni makubwa ya teknolojia yanafanyia kazi zake.
✒️ Kufika Marekani jamaa ngeli(kiingereza) haipandi alichofahamu tu ni kuchapa kodi (sio kuvaa vizuri wewe c'on) akapata kazi kampuni moja inaitwa WebEx.
✒️WebEx ni watengenezaji wa softiwea za kuwasiliana kwa njia ya Video kama ilivyokuwa Skype au Leo hii WhatsApp Video.
✒️ Akaendelea kufanya kazi WebEx. Mwaka 2007 kampuni moja iitwayo Cisco ikainunua WebEx kwa dola za kimarekani bilioni 3.2 ambayo kwa sasa mwaka 2019 ni kama dola bilioni 4. Shida kubwa waliokuwa nayo Cisco ni kwamba wateja hawakufurahia huduma zao. Kuna muda sauti ilikuwa mbovu, ubora wa video mbovu. Eric Yuan alisikiliza sana malalamiko ya wateja, cisco hawakusikiliza chochote.
✒️ Ndoto yake ilikuwa kufanya mambo kwa ubora wa viwango vya juu lakini kampuni aliyoifanyia kazi ilikuwa inazingua.
Mwaka. Yuan akaamua kuacha kazi na kwenda kuanzisha kampuni yake. Akaondoka na mainjinia 40 wa Cisco.
Mmojawapo kati ya watu walioondoka Cisco pia kwa baadae alikuwa jamaa anaitwa Dan Scheinman. Huo ulikuwa mwaka 201.
Jamaa akataka kutengeneza mfumo mpya utakaowawezesha watu kuwasiliana vyema kwa njia ya video ambao ni zaidi ya hule wa Cisco chini ya mwavuli wa WebEx. Akatafuta wawekezaji wakakosa, kwasababu walijua hawezi kulimudu soko make tayari kuna kampuni kama Skype, Apple, google na Cisco wako sokoni.
Akaongea na huyo jamaa Dan Scheinman, jamaa kwasababu alishafanya nae kazi na anamkubali sana akamsainia cheki ya dola 250,000 hiyo ni Aprili 2011.
Mwanzoni akawa anaiita kampuni aliyoianzisha kwa jina la Saasbee (usishangae jina lefu hata Amazon ilianza inaitwa Kadabrah)
Baadae akatafuta jina fupi kati ya haya 4; Hangtime, Poppy, Zippo na Zoom.
Hapo aliyekuwa CEO wa WebEx, Subrah Iyar naye akawekeza dola za Kimarekani 250,000 maana aliamini katika kipaji na maono ya Yuan
Akaajiri mainjinia wengi zaidi kutoka China maana wa Marekani alishindwa kufika bei. Wakaanza kutengeneza kitu kinaitwa Zoom. Agosti 22, 2012 wakafanikiwa kuizingua Zoom applikesheni inayoweza kuwasaidia watu kuwasiliana kwa njia ya video.
Zoom imekuja kupata soko kubwa katika msimu huu wa karantini ambapo watu wengi wamekuwa wakijifungia majumbani hivyo mikutano mingi imekuwa ikifanyika kwa njia ya mtandao wa Zoom. Watumiaji wamekuwa wengi sana na hivyo kuifanya kampuni hiyo kupiga pesa ndefu. Na pia kumfanya Eric Yuan kuwa bilionea. Ametajwa pia kuwa CEO namba 1 bora wa makampuni ya Teknolojia.
Unaambiwa kutoka Desemba 2019 mpaka sasa ongezeko la watumiaji wa Zoom ni mara 3 zaidi huku gawio la kampuni hiyo likikua kwa zaidi ya asilimia 50.
✍🏽Mwisho
Na Edius Katamugora
Creative Writer
Content Creator
0764145476
0 comments:
Post a Comment