Wednesday 27 May 2020

SIO KWAMBA HAUUZI BALI UMEKATA TAMAA





Colonel Sanders alianzisha KFC(Kentucky Fried Chicken) akiwa na umri wa miaka 65. Baada ya maisha kumpiga chini, kwake vyuma vilikuwa vimekaza zaidi ya kawaida. Maskini mzee huyu!

Baada ya kukaa chini na kufikiria anaweza kufanya kitu gani kinachoweza kumwingizia riziki alikumbuka kwamba mama yake alimfundisha kukaanga kuku vyema kabisa. Hivyo alijua anaweza kukaanga kuku vizuri zaidi ya mtu mwingine.

Colonel Sanders alianza kukaanga kuku na kwenda mlango hadi mlango kuuza kuku wake. Inasemekana alibisha milango Mara zaidi ya 1000 bila kupata mteja yeyote. Huo ndo ulikuwa mwanzo Wa KFC ambayo Leo imesambaa nchi karibia zote duniani. Ukifika pale posta KFC kunywa juisi ya buku tano jua kwamba mwanzilishi wake alianza kwa kusota hivyo.

Tatizo sio kwamba haujauza Bali umekata tamaa.

Najaribu kufikiria ni watu wangapi wameanza biashara Fulani baada ya kukosa wateja watatu au watano wakaacha biashara au kuuza bidhaa zao. Wengine watakwambia niliacha baada ya kupeleka biashara yangu kwa watu mia moja na sikupata mteja hata mmoja. Hebu fikiria Colonel Sanders angebisha milango mitano na kuacha! Jibu lipo wazi kwamba KFC isingelikuwepo.


Kwanini wewe umekata tamaa na kuuza?. Kwanini umekata tamaa baada ya mwaka mmoja wa biashara yako? Wataalamu wanasema biashara nyingi huanza kuleta manufaa baada ya miaka mitano. Kwanini unakata tamaa? Leo ni mbaya. Kesho ni mbaya zaidi. Kesho kutwa ni siku nzuri. Watu wengi hufa kesho jioni. Usikubali kufa kesho jioni kabla haujaiona kesho kutwa.

Ukitaka kukata tamaa kumbuka Colonel Sanders alibisha milango elfu moja bila hata mteja mmoja. Tatizo sio kwamba hauuzi, tatizo umekata tamaa.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

©  Edius Katamugora
0758594893
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: