Wednesday 27 May 2020

Kama Hautatui Matatizo, Wewe ni Tatizo


Kusingekuwepo na magonjwa madaktari na hospitali zisingekuwepo.
Baada ya watu kuchoka kuchomwa na miiba miguuni na kuumia, viatu viligunduliwa.
Jua na mvua vilipokuwa vikali kuna mtu akaona ni vyema kukawepo na kitu cha kupunguza vitu hivyo, mwavuli ukatengenezwa.
Wasingekuwepo wezi makampuni ya ulinzi yasingekuwepo.
Mafuriko yakitokea wenye makampuni wanapata miradi ya ujenzi wa nyumba na barabara.
Kuwepo kwa bahari na kuzama kwa meli kuliwafanya watu wafikirie kusafiri kwa ndege.
Matatizo mengi ndiyo yameibadili dunia, inategemea unayaonaje.

"Linapoandikwa kwa kichina neno 'matatizo' lina maana mbili: moja humaanisha "hatari" na nyingine humaanisha "fursa". Inategemea unaona nini katika lenzi ya matatizo," alisema John Firtzgerald Kennedy

"Kama hautatui matatizo basi wewe ni tatizo," anasema Sunday Adelaja. Rafiki yangu Padre Faustin Kamugisha aliandika kitabu kinaitwa Matatizo Si Tatizo, Matatizo ni daraja. Humo ametoa zaidi ya maana 26 za neno tatizo. Hauwezi kushinda au kumudu kitu kama haujui maana.

Napenda sana hekima hii ya Dkt. Beckwith aliyewahi kusema, "Nyuma ya kila tatizo kuna swali linajaribu kuulizwa. Nyuma ya kila swali, kuna jibu linajaribu kujitokeza. Nyuma ya kila jibu kuna tendo linajaribu kuchukua nafasi. Na nyuma ya kila tendo, kuna maisha yanajaribu kuzaliwa."

#Kijanawamaarifa
Edius Katamugora
Creative Writer
Content Creator
0764145476
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: