Friday 28 October 2016

Namna Ya Kutambua Kipaji Chako.

Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri na safari ya mafanikio katika maisha.



"Kila mtu amezawadiwa lakini baadhi ya watu hawafungui mabox ya zawadi zao" ni msemo wa kiingereza. Mpendwa msomaji Leo nitaongelea namna ya kutambua kipaji/vipaji ulivyo navyo. Kipaji ni uwezo binafsi ambao mtu huzaliwa nao. Kipaji kinaweza kuwa, kuimba,  kucheza,kuongoza. Mwandishi wa kitabu cha Think Big bwana Ben Carson anaingia ndani zaidi na kusema "hata kusoma kitabu na kuweza kung'amua Yale yanayosemwa ni kipaji pia".

Je  nitawezaje kujua vipaji vyangu?.
Hili ni swali ambalo kimsingi umekua ukijiuliza na kati ya watu wengi ni wachache ambao wameweza kujua vipaji vyao, wengine imewachukua muda mrefu kufahamu vipaji vyao.

Yafatayo ni  mambo ya kufanya hili utambua vipaji vyako.
1. Waulize rafiki zako.
Rafiki zako wa karibu,familia na ndugu ni watu ambao wanakufahamu wewe haswa, waulize watakusaidia kujua vipawa/vipaji vyako. Waulize maswali kama;
-Unazani kipaji changu ni kipi?.
-Madhaifu yangu ni yapi?.
-Kama nikitokea kwenye ukurasa wa  mbele(front page) wa gazeti litakuwa gazeti gani?.
Majibu utakayopata yatakusaidia kujua wewe haswa huna kipaji gani.

2.Vitu unavyopenda sana (passion).
Jiulize unapenda kufanya vitu gani ukiwa peke yako, kwani vitu unavyopenda vinaweza kukufanya wewe kufurahia hata kama utakutana na vikwazo. Mfano, Mimi napenda sana kusoma vitabu, na Nina mpango wa kuwa mwandishi wa vitabu, tayar I hicho ni kipaji.
Je  wewe  unapendelea kufanya vitu gani?



3.Wasikilize watu wanasema nini juu yako.
Watu wakikwambia "wewe ni kiongozi mzuri" au "unasauti nzuri" fata kile unachoambiwa. Kuna watu walinambia "edy una kipaji cha uandishi" Leo namiliki blog. Fata sauti za watu kwani ni sauti ya Mungu kwa kilatini wanasema "voces populi vox Dei"
Jambo lingine pia la msingi tusilazimishe vipaji ambavyo hatujapewa/hatujazawadiwa. Je  unamfahamu Hussein Bolt ni mkimbia mbio namba Moja duniani alijaribu kucheza mpira wa miguu na kushindwa. Michael Jordan pia mcheza kikapu bora duniani alikwenda kucheza mpira wa gofu lakini hakuwa bora. Cheza na kipaji chako.

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu Edius Katamugora.
Tuwasiliane: 0764145476.
Whatsapp: 0758594893.
Instagram; ediuskatamugora.
Fb:Edius Katamugora

Tukutane kesho kwenye makala nzuri kama hii.Asante
"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: