Saturday, 29 October 2016

Ijue Thamani Ya Muda.

Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri na safari yako ya kuyatafuta mafanikio katika maisha.

Leo hii nitaongelea umuhimu wa muda katika maisha yetu. "Tumepewa sekunde 86,400 kila siku, je umetumia muda gani kumshukuru Mungu?". Alisema William Arthur. Tumshukuru Mungu kwa kila muda anaotujalia kila siku.

"Uwa muda ukuue" no msemo wa kiingereza, je tunautumiaje muda wetu?. Tuutumie muda kufanya mambo yanayotujenga katika kila siku MPYA tujifunze mambo mapya "Anayeacha kujifunza kwa sababu amemaliza kusoma hawezi kufanikiwa" anasema Napoleon Hill mwandishi wa kitabu cha Think And Grow Rich. Hata kama tukiwa tupo katika likizo zetu za kikazi tuzidi kuutumia muda wetu vizuri sio kuweka miguu juu, kunywa na kusaza. Tajiri namba moja duniani ni miongoni mwa watu wanaotumia muda wao vizuri, kwa mwaka anachukua likizo ya mwezi mmoja, akiwa likizo huchukua begi la vitabu na kwenda mahali palipotulia na kuvisoma ili kuendeleza kampuni yake. Ndo maana Microsoft ni kampuni namba moja kwa ubora duniani.

Dr. Faustin Kamugishi kuhusiana na umuhimu wa muda alikuwa na haya ya kusema; "Ukitaka kujua umuhimu wa mwaka mmoja muulize mwanafunzi aliyerudia darasa. Ukitaka kujua umuhimu wa mwezi mmoja muulize mama mjamzito aliyejifungua mwezi mmoja kabla. Ukitaka kujua umuhimu wa siku moja muulize mwandishi wa makala za gazeti zinazotoka kila siku. Na ukitaka kujua umuhimu wa dakika moja muulize msafiri aliyechelewa kupanda Air Tanzania/ndege ya Mugufuli. Ukitaka kujua umuhimu wa sekunde moja muulize mwanajeshi katika medani za kivita".

Tuutumie muda wetu kwa mambo yanayojenga na ya kimaendeleo.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako Eddy Bide.
Tuwasiliane: 0764145476
Whatsapp:0625951842
Instagram; @eddybide

Tukutane kesho kwenye makala nzuri kama hii.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: