Thursday, 27 October 2016

Tuone Chanya Katika Kila Jambo.

Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kuwa haujambo na unaendelea vizuri na safari yako ya mafanikio. Nakushukuru pia kwa kuwa mdau na msomaji wa makala zangu kila siku, naomba uendelee na moyo huo.
Aliyevumbua miamvuli aliitwa mchawi. Watu waliona hasi katika miavuli. Aliyevumbua gari aliambiwa , "uwezi kuliondoa." Alipoliondoa aliambiwa "huwezi kulisimamisha." Akalisimamisha. Tuone chanya katika kila jambo. Katika milima tuuone uwepo wa mabonde na katika magonjwa tuuone uwepo wa afya.
Ukiwa unaendesha gari ukakwama kwenye msongamano wa magari mshukuru Mungu, kuna wenzako hawana hata mkweche wa baiskeli. Ukiwa unalalamika baada ya kula kwa kuosha sahani nyingi , mshukuru Mungu kwamba una aina nyingi za vyakula yaani mapochopocho na  una watu wengi wa kula chakula. Kama una nguo nyingi za kufua badala ya kulalamika kwamba ni Chafu sana mshukuru Mungu kwa sababu una nguo nyingi kuna wenzako wana nguo moja wanaiita kauka nikuvae.
Tegemea mazuri katika maisha yako na pia kuwa na matumaini, "matumaini hayamuui yeyote" ni methali ya Kongo. Ingawa matumaini hayaliwi kama chakula huwezi kuishi bila matumaini. "Matumaini ni nguzo ya dunia" ndivyo isemavyo methali ya kiafrika.
Je ni nitafanyaje ili niweze kuona chanya katika kila jambo?
Kutumi sheria ya ukiri chanya (The law of confirmation and affirmation). Hii ni kanuni ambayo hukuwezesha wewe kujinenea mazuri kila siku.
Affirmation
Ni kile kitendo cha wewe kuamua kunena maneno Fulani kila Siku ukiamka asubuhi, kwa mfano unaweza ukawa umeyaandika sehemu au hata kama hujaayaandika lakini ikawa ni maneno ambayo unayasema tu labda sababu umeyazoea kwa mfano "Leo ni siku nzuri sana nitafanya biashara, Leo najua nitashinda tu". Unavyofiri ndivyo ndio unavyojiwekea mazingira mazuri ya kuruhusu ubongo wako kuweza kuvutia mafanikio zaidi. Tofauti sana na mtu ambaye anasema "Leo tena, sijui itakuwaje Mungu saidia" haya ni mambo tofauti, hapana usiseme hivyo kiri mema "am the best" "am the winner" "I know I can do it" Mara zote kiri kushinda jisemee maneno ya ushindi.
Ni Mimi rafiki na ndugu yako Eddy Bide.
Tuwasiliane: 0764145476
Whatsapp; 0625951842
instagram;eddybide
Fb; eddy bide
Tukutane kesho kwenye makala nzuri kama hizi. Asante
"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

2 comments:

SONGA MBELE said...

Uko vizuri mkuu nmeipenda sana hiyo

Edius Katamugora said...

Pamoja sana kiongzi. Asante na karibu tena